AZAM FC imezidi kujitanua kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba SC jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam  ikitoka nyuma kwa bao 1-0.
Shujaa wa Azam alikuwa ni mshambuliaji kutoka Ivory Coast na mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, Kipre Herman Tchetche (pichani kushoto) aliyefunga mabao yote ya timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa.
Kwa matokeo hayo, Azam inatimiza pointi 23 na kujinafasi kileleni, ikiwazidi kwa pointi tatu Simba SC na Mbeya City katika nafasi ya pili.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Oden Mbaga aliyesaidiwa na Hamisi Chang’walu na John Kanyenye wote wote wa Dar es Salaam, hadi mapumziko timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1. 
Simba SC ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 21 kupitia kwa Ramadhani Singano ‘Messi’ aliyemalizia mpira ulioingizwa kutoka pembeni na Zahor Pazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hatimaye Mnyama mkali aliwa mchuzi na KICHECHE WA AZAM !

    ReplyDelete
  2. Mnyama alichomoka kwenye KISU siku ya Jumamosi ya tarehe 20/Oct/2013.

    Na sasa Mnyama kwa kuwa ni Mnyama akajisahau amejikuta tena KISU kipo kwenye koromeo lake !

    ReplyDelete
  3. Mnyama Kwishneyyyy !

    Kisu cha shingo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...