Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), limeiomba radhi Serikali ya Tanzania kufuatia taarifa waliyoitoa kwenye Mkutano wa 64 wa Kamati Tendaji (EXCOM) ya shirika hilo uliofanyika Geneva, Uswisi tarehe 30 Septemba hadi tarehe 4 Oktoba, 2013. Katika taarifa yao kuhusu Afrika, UNHCR ilieleza kuwa Tanzania imewafukuza Wakimbizi wa Rwanda na Burundi katika operesheni ya kuwaondoa Wahamiaji haramu inayoendelea nchini.
UNHRC imeiomba radhi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia barua yake ya tarehe 2 Oktoba, 2013. Barua hiyo imeandikwa na Mkurugenzi wa UNHCR Kanda ya Afrika Bw. George Okoth-Obbo kwenda kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Ame Silima aliyeongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo unaofanyika kila mwaka.
Katika barua hiyo, UNHCR imeeleza kusikitishwa na taarifa hiyo ambayo si ya kweli na imekiri kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikishirikiana kwa karibu na UNHRC katika ngazi zote kuhakikisha kwamba hakuna mkimbizi anayerejeshwa kwao katika zoezi la kuwakamata na kuwarejesha kwao wahamiaji haramu linaloendelea nchini Tanzania.
Aidha, Bw. Okoth Obbo ameeleza kuwa UNHCR na Jumuiya ya Kimataifa kwa ujumla inatambua na kuthamini kwa dhati mchango mkubwa ambao Tanzania imeutoa na inaendelea kuutoa katika kuwahifadhi wakimbizi wa mataifa mbalimbali kwa kipindi cha takribani miaka 40.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea kauli hiyo na kueleza kwamba inatarajia na inaamini kwamba UNHCR itaendelea kutoa taarifa sahihi zenye kutoa picha halisi inayoonesha namna Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyotekeleza wajibu wake kuwalinda na kuwahifadhi Wakimbizi kwa mujibu wa Sheria za nchi na mikataba ya Kimataifa ambayo nchi imeridhia.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
UNHCR tunajua Watanzania ya kuwa LAWAMA ZA KUWAFUKUZA WAKIMBIZI KUONDOKA TANZANIA hizi ni Kampeni chafu za Jirani zetu wa mashaka zaidi Jamhuri ya Rwanda.
ReplyDeleteKwani haikutosha Miaka yote hiyo tokea mwaka 1959 Ninyi bado mpo Tanzania tu?
Angalia Mkutano umefanyika kuanzia 30 Septemba-hadi 4 Oktoba na Barua ya kuomba radhi inaandikwa tarehe 2 Oktoba na Mkuu wa UNHCR Ndugu Obbo, ni kuwa ametambua wazi kabla ya Kikao kwisha huko Geneva-Uswisi ya kuwa madai hayo dhidi ya Tanzania ni ya Uongo mtupu !!!
Jamani wadau tumeomba serikali ya Tz iitake UNHCR itangazie ulimwengu kupitia CNN kuomba radhi ili kusafisha jina la Tanzania ambalo tayari wamelichafua. Je wameshafanya hivyo? Najua huyo Okoth ni mtani wetu ndio maana aliona achafue kwanza kasha aombe msamaha kimyakimya.
ReplyDeleteMdu wa Pili, UNHCR wanatakiwa watangazie Vyombo vyote vikubwa vya Habari vya Dunia nzima kuhusu Apologize hiyo.
ReplyDeleteVyombo vikubwa vya Habari Duniani:
-CNN: Marekani
-VOA: Marekani
-FOX News: Marekani
-ABC News: Marekani
-CBS News: Marekani
-BBC: Uingereza
-SKY News: Uingereza
-Radio Japan: Japan
-Al Jazira: Qatar
-Reuters: Uingereza
-Deutsche Welle: Ujerumani
-CCTV News: China
-Xinhua: China
Pia ni vigumu kupata maendelo kama ukiishi na Jirani asiye kutakia mema na ambaye mara zote ana kudharau na kukuhujumu kichini chini, vizabi zabina kuhusu Suala la madai ya Wakimbizi dhidi ya Tanzania ambao ni wa wapiga debe wa Kiafrika Majirani zetu nao watangaze. KBC-Nairobi na Radio Kigali-Rwanda.