Uongozi
wa Tawi la CCM - Moscow chini ya mwenyekiti wake Dr. Alfred Kamuzora unatoa
shukrani zake za dhati kwa Naibu Waziri wa uchukuzi Dr. Charles Tizeba kwa mchango wake wa hali
na mali kwa Tawi, tunamshukuru sana kwani mchango wake umeongeza imani ya
wanachama na kujua kuwa viongozi wa chama wako pamoja nao.
Katika kikao kifupi na viongozi
wa Tawi mwenyekiti amemuelezea naibu waziri Dr. Tizeba kuwa ni kiongozi mahili
kwani ni kiongozi ambaye mahali popote yupo tayari kukitetea na kukilinda chama
kwa kila hali. Huu ni ujasiri ambao ametuachia sisi kama viongozi wa Tawi
kusimamia itikadi na sera za chama mahali popote na wakati wowote.
Dr. Kamuzora alisema kuwa Dr.
Charles Tizeba ambae ni Naibu Waziri wa Uchukuzi ni mfano wa kiongozi wa kuigwa
kwani ni kiongozi asiyependa urasimu kwani ni muwazi na mtendaji na ambae
anakubali kusikiliza na kutoa ushauri na uamuzi pale ambapo uamuzi huo
unatakiwa kutolewa na yale yakufanyia kazi basi anayatolea maelezo.
Hii
ilibainishwa katika mkutano ambao Naibu Waziri aliufanya alipokutana na
watanzania pamoja na maofisa wa ubalozi wa watanzania jijini Moscow nchini
Urusi.
Wakati huo huo Dr. Kamuzora
amewataka viongozi wa Tawi kuiga mifano ya viongozi kama hawa wenye ujasili na
wasiopenda urasimu kama ilivyoonekana kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi Dr. Charles
Tizeba.
IMETOLEWA NA UONGOZI,
TAWI LA CCM MOSCOW
Tawi la Republican kufunguliwa next month hapa Uvinza. Please board the train to Kigoma and drop at Uvinza Railway Station. Chipukizi watakuwa hapo kuwapokea. Tunashukuru wananchi wote kwa michango yenu.
ReplyDelete