Naibu Katibu mkuu UWT Taifa ndugu Eva Kihwele akizungumza na wanafunzi wa Ikuwo Sekondari
Na Edwin Moshi wa
Globu ya Jamii, Makete
Umoja wa wanawake wa CCM Tanzania (UWT) umeahidi kutoa solar Panel moja yenye thamani ya zaidi ya tsh laki nane kwa shule ya sekondari Ikuwo iliyopo wilayani Makete mkoani Njombe
Ahadi hiyo imetolewa na Naibu katibu mkuu wa UWT Taifa Eva Kihwele wakati alipofanya ziara katika shule hiyo jana ambapo pamoja na mambo mengine alikagua mabweni ya wasichana yaliyopo shuleni hapo
Akisomewa taarifa ya shule hiyo na Mkuu wa shule alisema pamoja na mafanikio lakini wana upungufu wa sola kwa ajili ya kutoa nishati ya umeme ambayo itawasaidia kuongeza ufanisi na utendaji kazi shuleni hapo ikiwemo kujisomea jambo lililoigusa UWT na kuamua kutoa msaada huo
Mbali na kuahidi kutoa sola hiyo, pia kiongozi huyo ametoa shilingi laki moja kwa ajili ya sukari ya wanafunzi hao ambao wanalala shuleni hapo
Akizungumza na wanafunzi hao Naibu Katibu mkuu UWT Taifa Bi Kihwele amewataka kuzingatia masomo kwa kuwa watoto wengi wa kike wamekuwa hawafikii malengo yao, na kuwataka wao kuwa mfano wa kuigwa kwa kusoma kwa bidii hadi wafikie chuo kikuu, ili badae wawe na kazi nzuri itakayowasaidia kuingiza kipato chao cha kila siku
Viongozi wa kitaifa wa UWT wapo wilayani makete kwa siku tatu kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kukagua miradi ya maendeleo na kuchukua changamoto mbalimbali za wananchi ili kuzipatia ufumbuzi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...