Wanafunzi wa kike wa Ikuwo sekondari kwa sasa wanalala hapa kama ilivyoshuhudiwa na mtandao huu.
kama kawaida wamepanga magodoro yao chini kwa raha zao
Mkuu wa shule ya Ikuwo Sekondari akifafanua jambo kwa mwandishi wetu.
=====
Na Edwin Moshi, Makete
Kutokana na idadi ya wanafunzi wengi wa kike wilayani Makete mkoani Njombe kukatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupata mimba, shule ya sekondari Ikuwo imeonesha kukerwa na tatizo hilo na kuamua kuchukua hatua za awali za kupambana nalo
Mwandishi wa mtandao huu alifika shuleni hapo na kukuta wanafunzi wa kike wote wakiwa wanalala shuleni hapo licha ya mabweni hayo kukumbwa na changamoto ya ukosefu wa vitanda
Mkuu wa shule hiyo akizungumza na mwandishi wetu amesema kutokana na tatizo hilo kuzidi kuwa kubwa, uongozi wa shule na wilaya kwa ujumla walikubaliana wanafunzi hao watandike magodoro sakafuni waendelee kulala mabwenini humo, wakati serikali ikiendelea kutafuta vitanda kwa ajili ya mabweni hayo
"Kwa wakati huu ambao tunasubiri kuletewa vitanda na serikali, tumeona ni bora wanafunzi hawa wa kike waendelee kulala chini kwa kutandika matandiko yao ili kupunguza ukubwa wa kupata mimba pamoja na kufeli" alisema mwalimu mkuu huyo
Mtandao huu ulipenya kwenye mambweni hayo na kushuhudia magodoro yaliyotandikwa kwa unadhifu wa hali ya juu, ambapo wanafunzi hao wanalala kwa muda wakisubiria vitanda
Hivi karibuni katika mahafali ya kidato cha nne Iwawa sekondari afisa elimu sekondari wilaya ya Makete Jacob Meena alikaririwa akisisitiza wanafunzi wa kike wa shule hiyo waanze kulala shuleni kuanzia mwakani hata kama mabweni hayana vitanda kama wanavyofanya Ikuwo sekondari
Wewe unazungumzia wanafunzi kulala chini si uende muhimbili uone wagonjwa wanakolala?
ReplyDeletewakifeli watasema kwa sababu walilala chini. hapana.
ReplyDeletekulala chini ndo ukumbusho wa kusoma kwa bidii ili usilale chini ukihitimu.
MDAU wa kwanza hapo juu nakubaliana na wewe hili sio tatizo ukilinganisha na wagonjwa pale muhimbili au takriban hospitali zetu zote hapa nchini
ReplyDeletena wenye kitanda hawana godoro wanalalia waya ...ukitaka ukweli wa haya tembelea hospitalini
Kulala chini si tatizo naona, hivi mnajua nchi kama Japan kulala chini ndio mila yao! Unaenda kwenye hotel za kimataifa unakuta godoro limewekwa chini. Kinachohitajika ni mazingira bora, nikiangalia picha hizo sioni la kuwafanya watoto hao kushindwa kusoma eti kwa kisingizio cha kulala kwenye godoro zilizowekwa chini.
ReplyDeleteMbona bweni zuri tu ndani. kulala chini hiyo mbona kawaida tu, kuna baadhi ya shule za secondary, wala hazijielewi mradi bora liende, wanafunzi bwenimoja wamerundikana utazani magunia, hata vitanda havieleweki, ni msongamano tu, kulala Kwa kiubavu bavu, si ndio kwenye nchi zetu tulivyo,ikiwa mahospitani wanalala chini ndio itakua mashuleni? mradi book linaendelea kiugumu ugumu tu
ReplyDelete"...kulala chini hiyo mbona kawaida tu" duniani!
ReplyDeleteNdio, kiafya, ni vizuri kulala chini kuliko kitandani!