Mwandishi wa habari wa Kituo cha ITV na Redio One, Ufoo Saro, bado yupo katika Chumba cha Dharula katika Hospitali ya Muhimbili, akiendelea kupatiwa matibabu kufuatia tukio la kupigwa risasi na mtu anayedaiwa kuwa Mchumba wake alfajiri ya leo huko maeneo ya Kibamba, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. 
 Kamanda Suleiman Kova, akizungumza na waandishi wa habari wakati akiwa eneo la Hospitali ya Muhimbili leo mchana alipofika kujua kinachoendelea juu ya tukio hilo na maendeleo ya mgonjwa. 
 Baadhi ya waandishi wa habari waliofika Hospitalini hapo leo kwa ajili ya kujaribu kumuona, lakini haikuwezekana kuruhusiwa kutokana na mgonjwa huyo kuendelea na matibabu katika chumba cha dharula.
 Baadhi ya wafanyakazi wenzake wa Redio One na ITV, wakiwa Hospitalini hapo wakisubiri kumuona mgonjwa.
 Wapigapicha nao walipozi katika anlge ya peke yao wakivizia kunasa picha ya mgonjwa huyo wakati akitolewa katika chumba cha Dharula.Picha na Sufiani Mafoto Blog.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...