Baadhi ya washiriki wa warsha ya pamoja kwa wadau wa sekta ya nishati wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi  (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano wa saba uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency  iliyopo jijini Dar es Salaam. Serikali imekamilisha utafiti katika  vituo 52 vya kutoa umeme wa joto ardhi (geothermal) na ifikapo mwakani uchimbaji wa umeme huo utaanza katika vituo vitatu vilivyopo katika mkoa wa Mbeya, wilaya ya Rufiji na katika ziwa Natroni lililo  mkoani Manyara.
 Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi  (kulia) akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng. Ngosi Mwihava (katikati) wakati wa warsha ya pamoja ya siku moja kwa wadau wa sekta ya nishati iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency  iliyopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kamishina wa masuala ya Nishati na Mafuta Eng. Hosea Mbise.
 Washiriki wa warsha ya pamoja kwa wadau wa sekta ya nishati wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi  (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano wa saba uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency  iliyopo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi  (kushoto) akiongea na Dk. Lennart Larsson (kulia) mara baada ya ufunguzi wa farsha ya pamoja ya siku moja kwa wadau wa sekta ya nishati iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency  iliyopo jijini Dar es Salaam.
 
 Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi  akifungua warsha ya pamoja kwa wadau wa sekta ya nishati leo katika Hoteli ya Hyatt Regency  iliyopo jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo wa saba uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency  mambo mbalimbali yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na masuala ya mafuta, umeme na gesi.
Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi (kulia) akiongea jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng. Ngosi Mwihava wakati wa  warsha ya pamoja kwa wadau wa sekta ya nishati iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Serikali imekamilisha utafiti katika  vituo 52 vya kutoa umeme wa joto ardhi (geothermal) na ifikapo mwakani 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. SEKTA YA NISHATI:

    Hii ndio Sekta itakayo watoa kamasi KENYA, RWANDA na UGANDA na kuisoma namba za nyuma TANZANIA!

    UN na Mashirikisho ya Maenddeleo inasema ya kuwa NCHI YEYOTE YA DUNIA ITAKAYOWEZA KUONGEZA UPATIKANAJI WA UMEME WA UHAKIKA KWA KILA 1.08% ITAENDELEA KWA 10% !

    TUELEWE TANZANIA INA VYANZO VINGI MNO VYA NISHATI KTKT HII EAC KULIKO NCHI ZINGINE NA KWA WINGI MKUBWA KAMA:

    -GEOTHERMAL (inayo zungumziwa hapa)
    -URANIUM
    -GAS LNG
    -COAL
    -SOLAR VAST SKIES

    HIVYO NI PAMOJA NA SEKTA ZINGINE ZITAKAZO CHANGIA NI WAZI HAWA JAMAA WA 'COALITION OF THE WILLING' KWENYE HII EAC WANALIJUA HILI NDIO MAANA HAWAISHI VIKAO!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...