Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akisistiza jambo kwa watangazaji wa vipindi vya redio mbalimbali (hawapo pichani) kuhusu vigezo na masharti vinavyotakiwa kufuatwa kwenye promosheni mpya ya Airtel ya "Mimi ni bingwa" itakayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kushinda tiketi 2 kila wiki za kwenda kushuhudia mechi mbalimbali za timu ya Manchester United na mamilioni ya pesa kila siku.Kulia kwake ni ofisa wa matangazo wa Airtel Bw. Abdallah Gunda.
Toka kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airte Tanzania Bw Jackson Mmbando akibadilishana mawazo na watangazaji wa kipindi cha jahazi bw Musa Huseni (kati) na Ephraem Kibonde mara baada ya mkutano maalum na watayarishaji na waandaaji wa vipindi mbalimbali vya redio kwa lengo la kuwaeleza vigezo na masharti vinavyotakiwa kufuatwa kwenye promosheni mpya ya Airtel Mimi ni bingwa" inayowawezesha wateja wa Airtel kushinda tiketi 2 kila wiki za kwenda kushuhudia mechi mbalimbali za timu ya Manchester United na mamilioni ya pesa kila siku
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...