AFRICAN STARS ENTERTAINMENT (ASET) kupitia katika Bonanza lake inaloliendesha kwa kila Jumapili Leaders Club Kinondoni, imeamua kuboresha bonanza hilo kwa kuongeza timu za mpira wa miguu za macamp. 

Timu za Macamp zilizoongezwa, ni zile camp ambazo zinashabikia bendi ya African Stars “Twanga Pepeta”.

Timu za Camp ambazo zilizoongezwa ni pamoja na Daladala Camp, Wakutengwa Camp, Freedom Camp, Makono Camp, Garage Nchangani, Msisiri camp,  Masella Camp, Ashanti camp, Usher Family Camp na Super Camp. Mechi zinazozihusu camp zitaanza saa saba mchana mara baada ya kumalizika kwa mechi za awali zinazoihusu timu za maveterani.

Nia kubwa ya kuziongeza timu hizi za macamp, ni kuongeza burudani inayopatikana katika bonanza la kila jumapili Leaders Club. Sambamba na hilo pia ni kutambua mchango wa macamp wanaotupa kwa mingi, hivyo tulionelea kuingiza timu zao za mpira wa miguu.

Matayarisho yote muhimu kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa ushiriki wa timu za macamp katika bonanza la kila Jumapili hii tarehe 17-11-2013  yamekamilika na ufunguzi huo rasmi unataraji kufunguliwa rasmi na Mkurugenzi wa ASET Bi Asha Baraka. Kama ilivyo kawaida mara baada ya mechi za mpira wa miguu kumalizika Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” inatarajiwa kutoa burudani kali kwa mashabiki watakaohudhuria ufunguzi huo rasmi.  

ASHA BARAKA
MKURUGENZI MTENDAJI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...