Mamlaka
ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA) imehamasisha uwekezaji
katika viwanda vya kubangua na kusindika korosho na kusema kwamba iko
tayari kupokea wanaotaka kufanya hivyo na kuwasaidia katika maeneo yake
ya uwekezaji.
Imesema
Tanzania bado haina viwanda vya kutosha vya kubangua korosho hali
mabayo inarudisha nyuma sekta ndogo ya uzalishaji zao hilo.Mkurugenzi
wa Uhamasishaji Uwekezaji na Huduma wa Mamlaka hiyo, Bi. Zawadia
Nanyaro aliwaambia waandishi wa habari baada ya mkutano wa sekta hiyo
ndogo ya kilimo hivi karibuni jijini Dar es Salaam kuwa viwanda vya
kubangua korosho bado havitoshi na hiyo inarudisha nyuma maendeleo ya
uzalishaji zao hilo muhimu.
“Zao
hili ni moja kati ya mazao muhimu yakiwemo ya kahawa, tumbaku, pamba na
Korosho yenyewe ambayo ni muhimu kwa uchumi wa nchi,akini
linakabiliwa na tatizo la uchache wa viwanda,” alisema.Alisema
mamlaka yake inahamasisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kutumia
programu za mamlaka hiyo kuwekeza katika viwanda vya kubangua korosho
ili kuondoa tatizo hilo na kukuza uzalishaji.
Alifafanua
kuwa wawekezaji wa nje wanapofika kuwekeza wanasaidia wawekezaji wa
ndani kupata maarifa, ujuzi na teknolojia na hiyo ndiyo njia ya kuleta
maendeleo. “Tunashukuru
mkutano huu wa wadau kufanyika kwa vile tumeweza kutumia fursa hiyo
kutoa elimu kwa washiriki kutumia fursa za uwekezaji ndani ya programu
za mamlaka,”alisema Bi. Zawadia.
Aliongeza
kusema kuwa njia ya kuondokana na hali duni ya uzalishaji na vipato ni
kutumia fursa zilizopo ili kujikwamua kwa faida ya taifa zima. Alisema
zaidi ya asilimia 90 ya korosho inayozalishwa hapa nchini huuzwa bila
ya kuongezewa thamani na kusababisha wakulima kushindwa kupata faida
stahiki.“Nchi
haitaweza kupiga hatua na wakulima watabaki kuwa masikini kama nchi
itaendelea kuuza korosho bila ya kuongezewa thamani,” alisema na
kuongeza kuwa EPZA inalenga kuondokana na tatizo hilo.
Alisema
mamlaka hiyo inahamasisha uzalishaji na uongezaji thamani mazao ili
kujiepusha na uuzaji mazao yakiwa ghafi katika masoko ya nje.Kwa Upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Mungano Vyama
vya Wakulima wa Korosho Afrika (Africa Cashew Nuts Alliance), Bw.
Maokola Majogo alisema kuna kila sababu ya serikali kushirikiana na
wadau wa korosho kupata masoko ya uhakika
“Zao
hili ni muhimu sana kwa mikoa ya kusini katika kujipatia vipato...ni
lazima lipewe kipaumbele na masoko yake yawe ya uhakika,”alisema.Alisema
anamuomba waziri wa Viwanda na Biashara kutembelea viwanda vya
kusindika ili kujua matatizo yanayowasibu na kuchukua hatua ya namna ya
kuondokana na matatizo hayo.
Aidha
alisema sekta hiyo inakabiliwa na tatizo la mikopo kuwa na riba kubwa
na kusababisha shughuli za uzalishaji korosho katika mnyororo wake
kushindwa kufikia malengo yake.Kwa
mujibu wa Waziri wa Kilimo, Chakula na Masoko, Bw. Christopher Chiza,
mikoa hiyo ya kusini ina uwezo wa kuzalisha tani 154,000 za korosho na
mipango ya serikali ni kuona inafikia tani 300,000 kwa mwaka.
“Sasa
hivi tunazungumza tufike sehemu mazao ya kahawa, tumbaku, pamba na
korosho yanapopata matatizo ya masoko ya nje basi yaweze kupatiwa ruzuku
kuzuia kuporomoka kwa uzalishaji,” alisema.Alisema
mikakati ya namna hiyo itawezesha uzalishaji kutotetereka ili nchi
iweze kupiga hatua kwa sababu mazao hayo ni muhimu kwa uchumi.
Mkutano
wa wadau wa sekta hiyo ndogo ya Kilimo ulifanyika jijini Dar es Salaam
ukishirikisha wadau mbalimbali kupata fursa ya kujadili njia za
kuendeleza zao hilo.



Mbona wametuachia umaskini huku Bagamoyo, ahadi za kutulipa maeneo yetu sasa mwaka wa saba. Kesho kesho ...kesho.......... Leo eti wanahamasisha uwekezaji hivi hamjisikii vibaya kusema uongo.
ReplyDelete