GoldenBush Veterans, wazee wa amsha amsha watakuwa uwanjani kwao yaani Saint James Park “Kinesi” kurudiana na timu ngumu kabisa Kivukoni veterans, ikumbukwe kwamba mechi ya kesho itakuwa ni game 3 kukutana na hawa jamaa ambapo mechi mbili zote Golden bush tulikubali vipigo viwili mfululizo, lakIni game ya pili tulifungwa kwasababu wachezaji wengi walikuwa na wa timu ya Wahenga.

Kesho tunatarajia kushushaa kikosi kizito sana ili kutoa kipigo cha haja na kuondoa kabisa dhana iliyojengeka huko Kigamboni kuwa timu yetu ni mbovu au ni vibonde.

Game itaanza saa mbili kamili asubuhi lakini milango ya uwanja wa Saint James Park iko wazi kuanzia sasa hivi kwa wale wanaotaka kuwahi siti za mapema. Timu yetu iko kwenye moody nzuri sana  ya ushindi, tumetoa vipogo vya 4-1, 3-1 kwa muda wa wiki tatu mfululizo, sifa ziende kwa bench la ufundi likiongozwa na Madaraka Selemani, Herry Morris kwa kazi yao nzuri sana.

Timu yetu sasa hivi iko Kampini Star light Hotel ili kuweka mazingira mazuri ya ushindi.

Pamoja na yote hayo, game ya kesho tutaitumia kumtambulisha mchezaji wetu mpya kabisa bwana Shaffih Dauda.

Karibu sna, njoo wewe mwanao ili upate burudani kutoka kwa wachezaji wenye records za kuwa man of match katika henzi zao hapa nazungumzia, Onesmo Waziri, Waziri Mahadhi, Abuu Mtiro, Yahaya Issa, Salum Athuman, Salum Swedi, Said Swedi, Steven Marash, Majaliwa Mwaigaga, Hamis Hassan Msamba, Katina Shijja na wengine lukuki.

Aanteni kwa kunisiliza.

Onesmo Waziri “Man of the Match”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...