Kaka Issa,
Kwa heshima na taadhima naomba utuwekee kwenye Globu ya Jamii  mjadala  huu wa Umiliki wa silaha kama unazingatia mahitaji,na kama taratibu zinazingatiwa,au masharti yamekuwa laini sana kiasi cha kwamba hata vichaa wanamiliki silaha kihalali.
Hii ni kutokana na mwendelezo wa mauaji ya raia wasio na hatia kutokana na dola kushindwa kudhibiti uuzaji wa silaha.Kwa mfano tukio la ufoo saro,na tukio la ilala bungoni.Na kama ipo haja ya kuunda tume kuchunguza kama kiila mmiliki wa silaha alifuata taratibu zote za kuhojiwa kuanzia ngazi ya mtaa mpaka kamati zote za ulinzi ambao huthibitisha kuwa mwombaji anastahili apewe silaha.
Maneno yanayoenea mitaani kuwa ni rushwa ndio hutumika kiasi cha kwamba kuna middlemen wenye kazi hii kutafita vibali na hatimaye mwombaji kuambiwa aendee kitabu chake sio jambo la kuvumiliwa.Kwa nini tumefika hapa tulipo?Je wamiliki wote wa silaha wanajua namna ya kuzitumia?      
Mdau Dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. HUO MJADARA UNAHUSU MAREKANI SIO TANZANIA, KWANI Dr. MVUNGI ILIMUUA SILSHA KAMA HIYO UNAYOONYESHA HAPO, KWA TANZANIA UNGEWEKA MAPANGA NDO YANAYOUA WATU SIYO HIYO BERETTA 10+. NEXT TIME WEKA HIYO SILAHA YAKO KATIKA BLOG ZA MAREKANI, HAO VICHAA WAKO SI WANAAZIMA TU KAMA WANAUA KWA SILAHA.

    ReplyDelete
  2. Sheria ya Umiliki wa Silaha Tanzania inavurugwa na kukomaa kwa rushwa na pia taratibu hazifuatwi ipasavyo.

    1.Umiliki wa Silaha unapattikana kulingana na urefu wa mkono wa anaye omba umiliki na sio Kanuni na Taratibu za umiliki kukamilika.

    2.Jambo baya zaidi ni kuwa ktk nchi nyingi duniani, umiliki wa Silaha unednana na upimaji wa Afya ya akili ya mmiliki wa silaha kitu ambacho Mamlaka za Tanzania zikishatoa silaha inakuwa ndio kimoja!, muhusika akiwa Taahira Mamlaka zinakuwa haziwajibiki kufuatilia mustakabali wa mtumiaji wa silaha baada ya kusaini na kupewa silaha.

    Mamlaka inasubiri matokeo ya maafa takayo fanya mmiliki wa silaha kama ilivyo tokea kwa suala la Mushi(Ufoo Saro) na hili la sasa la Munisi(Binti Alfred)

    ReplyDelete
  3. INABIDI TUANGALIE NANI ANASTAHILI KUMILIKI SILAHA,ENZI ZA MWALIMU SILAHA HAZIKUZAGAA KAMA ILIVYO SASA.NA WANAOIDHINISHA MTU KUMILIKI SILAHA WANAHAKIKI KAMA MUOMBAJI KAFUATA TARATIBU ZOTE?

    ReplyDelete
  4. Sitaki kuamini hoja inaletwa kwa misingi ya fikra. Taratibu zipo name zinafuatwa. Matukio hayahusiani name umiliki. Fanya utafiti ujenge hoja. Naungana na mdau Tz hoja Hii haina uzito. Pengine unastaajabishwa na wahusika. Mlinzi kujishuti akiwa doria unaielezeaje? Tujenge hoja zenye uhalisia

    ReplyDelete
  5. Mimi nakubaliana na mdau aliye leta hii hoja, ametoa mifano miwili (Ufoo na tukio la Ilala) ila ni wengi wamesha uliwa kwa silaha hizo za moto. Iko haja kabisa swala la umiliki wa silaha lichunguzwe, tusisubiri mpaka hali izidi kuwa mbaya. Na kama tukigundua hatuna uwezo wa ku control matumizi ya silaha (coz ulinzi wa nchi unapaswa uwe wa hali ya juu raia wanapo ruhusiwa kumiliki silaha kitu ambacho hatuna) basi tusimilikishwe silaha.

    Kama ulinzi wa nchi siyo imara kuzuia wana nchi wasi katwe mapanga na wasi mwagiwe tindi kali je watu wakiendelea kumilikishwa silaha za moto/bunduki itakuwaje!!??

    ReplyDelete
  6. Ukweli matukio ni mengi Ila sidhani Kama Tume zitasaidia, Hebu twende Iringa, samahani lakini wahehe wana hasira sana mpaka kujidhuru wenyewe je tuunde tume? vivyo hivyo wakurya wana hasira za kuchinjana. Matukio ya mauaji yasiyohusisha bunduki ni mengi kuliko ya silaha nyingine (visu mishale mashoka majembe mapanga mitwangio moto etc etc etc).
    Kwa mfano suala la Usaro, polisi walisema ile silaha ilikuwa inamilikiwa kihalali na muuaji... sasa inakuwaje.... mmiliki halali ameua. cha kiujiliza kwani aliichukua jana yake akafanya tukio kesho yake? if he owned it for sometimes and he didnt kill anyone why that material day? Normaly Arms renewal inamtaka owner aende kurenew personally sababu yake ni pamoja na kumfanya msajili aone current status ya owner, ana nguvu ya kuhimili mshindo? anaona? kiafya yukoje amekuwa frustrated? and so on. some few months back kuna mtu aligonga watu wakiwa Bar Makusudi, je na hilo tulifanyeje? yeye katumia gari kama silaha, amemiliki magari for years hakufanya hivyo why that day.... inaoneka kuna hali ya watu kukata tamaa ndiyo maana wanajiua after that, mimi nadhani some few issues zingekuwa adressed kwenye kerenew silaha. cheti cha daktari kuonyesha status ya mmiliki wa silaha. mgonjwa wa magonjwa sugu ikiwepo ukimwi anakuwa kwenye hali ya kukata tamaa... sina maana kuwa mwenye ukimwa forexample hahitaji ulinzi, ila awe monitored. Visual and mental checkup,

    ReplyDelete
  7. Inabidi uende Tarime ukaangalie jinsi watu wanavyouana kwa mapanga ambayo ni asilimia kubwa kulika matumizi ya Pistol. Kama ni uchunguzi ungewekwa kwenye visu, bisibisi, boda boda na mapanga ambayo ndio yanauwa kwa kasi ya ajabu Tanzania.

    ReplyDelete
  8. Nafikiri iko haja ya serikali kuelekeza sera na mkazo kwenye kuimarisha usalama wa raia kwa siraha kumilikiwa na vyombo vya usalama na kuimarisha mfumo wa kupata taarifa za uharifu kupitia ulinzi shirikishi wa jamii.
    Sera hii ya kumilikishwa siraha kwa nchi yetu ni muhimu kamati ya ulinzi na usalama ikaiangaliwa tena kwani ni kuiga na kutekeleza sera za nchi za magharibi ambazo lengo lao kubwa ni kupata soko la siraha zao katika nchi zetu.
    Mimi ninaamini na nina imani kubwa na vyombo vyetu vya usalama ukiachana wachache wasio waadilifu ndani ya vyombo hivi kuwa ndio wanaoweza kuhakikisha usalama wa raia kikamilifu. Umilikishaji wa silaha kwa raia ni kuongeza changamoto ya kiulinzi na pia kuhakikisha matumizi sahihi ya silaha hizo.
    Mfano mzuri tujinzo nchi jira kaskazini mwa TZ, ambao awaili walikuwa na nia nzuri ya kuwamilikisha Wafugaji wao silaha kwa lengo la kujilinda na uvamizi wa mifugo yao lakini hivi sasa silaha hizo hizo zimegeuka na kuanzisha vita kati ya kabila na kabila na hata zimetumika kuua askari wao wa usalama. It is true new thinking provides New possibilities, Lakini ni muhimu pia kuchukua tahadhari na kujifunza kwa kina juu ya mawazo hayo mapya.
    Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.
    THANKS

    ReplyDelete
  9. Kuna wezi wanaua watu kwa kutumia silaha za moto, hawajakamatwa hivyo haijulikani kama ni silaha zilizosajiliwa na wanazimiliki wao kihalali au ni za kutoka nchi zenye matatizo ya vita.. wao wanazikodisha tu au ni za wamiliki halali ambao wanawakodishia majambazi mimi nadhani kuna haja jamii kushirikiana na serikali/polisi kwa kuwa na kituo maalum ambacho say kama utamwona mtu say yuko bar ameweka silaha yake mezani ukazichukua hizo detail kisiri ukareport police wamchunguze. maana japo silaha ni kwa ajili ya personal and propert protection kwa kesi hiyo hapo juu sio sawa. loose handling ya silaha ndiyo inalead kwa matukio mabaya... Tanzania have very good control on arms, tafuta watu wangapi wameomba na hawajapata vibali kwasababu hawakidhi vigezo.., ila tu cha kujua ni kuwa mambo yanabadilika, unayemjua leo inawezekana miaka mitatu ijayo akawa amebadilika sana... hivyo periodical personal history update ni ya muhimu sana kwa kesi hii.
    Ninachijua mimi silaha inatakiwa iwe very private kwa mmiliki, hii ni kwa usalama wake, ukiifanya public vibaka wakija wanaitaka kwanza... na wakiichukua inakuwa ready for use illegally hapa tuwe waangalifu

    ReplyDelete
  10. Jamani siyo kweli silaha za moto zinaua kuliko silaha nyingine kama mapanga na sime. Pia siyo kweli nchi za ulaya zinapima akili kwa wale wote wanaomiliki silaha. Mimi binafsi nimeishi huko for over 15 years na nilikuwa nafanya kazi za kuuza kwenye duka la silaha na hakuna kipengele kama hicho cha kupima akili. Kinachofanyika ni kufika dukani unanunua na wale wanajaza form fulani ambazo hutumwa electronically kwa kufanya kitu kinaitwa background check, baada ya hapo utaitwa kwa usaili na akili yako itapimwa kwa maswali utakayoulizwa the same process inafuatwa hapa kwetu. Hakuna tofauti hata moja ukishindwa kujibu maswali hata hapa TZ hupewi silaha. Wadau tusipende kudanganyana na kutoa mifano ya nchi za nje kama wengine hatujaishi huko. Kule Marekani silaha huuzwa hata kwenye PONY SHOP na utaratibu wake ni sawa na hapa TZ huwezi ichukua silaha hadi upate clearence ya polisi nyie mlioko huko mnataka kutudanganya kama siyo nao hatujawahi piga box?
    Sheria zipo sahihi kabisa za umilikishwaji tatizo mtumiaji mwenyewe.

    ReplyDelete
  11. Si kweli silaha za moto ndo zinaongoza kwa kuua watu TZ. Kumiliki silaha ni haki ya kila MTZ anayefikia viwango stahiki.
    Dr Mvungi hakuuwawa na silaha ya moto ni mapanga tu!, imagine yule Lecturer wa CBE laiti angekuwa hana silaha nini kingemtokea dhidi ya wale majambazi yaliyomvamia usiku?
    Naomba tusichanganye mada hapa suala siyo umilikishwaji suala ni matumizi yake baada ya kuipata. Unapopatiwa silaha unafundishwa na sheria iko wazi kabisa kuhusu umiliki wake na utunzaji, ukiamua abuse jua utapata shida mwenyewe. Kesi ya UFUSAROO na hii ya juzi pale ILALA isitumike kabisa kuwanyima haki Watanzania wenye niya nzuri ya silaha kumiliki.
    Kuna radio moja kila jioni kupitia mtangazaji wake mropokaji sana amekuwa akiendesha campaign against umiliki wa silaha. Hiyo haipendezi kabisa kwani umiliki wa silaha ni haki ya kila Mtanzania anayefikia vigezo vilivyoweka na atakayekwenda kinyume ataadhibiwa kwa mujibu wa taratibu na sheria zilizowekwa. Ni ujinga uliokithiri kuanza kufanya camaign kuilaumu jeshi letu la polisi kuhusu umilikishwaji, kwani wanavyokupa wanasema ukaitumia kupiga watu kwa mambo yako ya WIVU? unaambiwa kabisa hiyo itakulinda dhidi ya UJAMBAZI na unaelekezwa nini ufanye pindi wanapokukabili, ukienda kinyume ni kivyako na ni msala wako mwenyewe. Wadau tuache laumu jeshi letu la polisi wakati linafanya kazi nzuri kabisa.

    Mbona hatusemi kuhusu wale madereva wanaoua watu kwa ajali zinazoepukika? hiyo si ku-abuse leseni zao za udereva? Wanaua wangapi? zile bodaboda nazo je? tunapigia kelele silaha kwa case 2 wakati wangapi wanakufa kwa ajali za kizembe barabarani na wengine hata kuachwa vilema?

    ReplyDelete
  12. Mchangiaji no 4umeleta hoja ya mauaji kwa visu na mapanga,visu na mapanga kumiliki huhitaji kibali wala hujazi fomu,hapa hoja ni silaha ambayo kuimiliki unahitaji kuwa screened kuanzia kwenye kitongoji unachoishi,Gabriel sidhani kama alikwenda physically kuhojiwa kabla ya kupewa silaha,haya hata polisi kituo cha pangani waliarifiwa vitisho lakini hawakuchukua tahadhari mpaka mauaji yametokea ndipo wakaja kuchukua gari walilopanda waliouwawa,hivi ni vichekesho kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.

    ReplyDelete
  13. KUNA MHESHIMIWA MMOJA ALIPANDA NA BASTOLA JUKWAANI,KWENYE MKUTANO WA HADHARA WA CHAMA,NI NANI ANAJUA KAMA ALIPOKONYWA SILAHA JAPO ALIHOJIWA,KWENYE MKUTANO UNAENDAJE NA BASTOLA?UKIVUNJA KANUNI ZA UMILIKI WA SILAHA UNAPOKONYWA NO DISCUSSION,JE MABISHOO WANAOJIONYESHA KUWA WANAMILIKI SILAHA
    WANGAPI WAMEPOKONYWA?

    ReplyDelete
  14. utekelezaji wa hoja kama ilivyowasilishwa si rahisi kwani mtoa hoja anahusisha kufanya sychological test kwa wamiliki wa silaha kitu ambacho si rahisi.kumbuka hata mataifa yaliyoendelea ie, USA pamoja na mifumo na taratibu nzuri walizonazo bado wameshindwa kucontrol hilo, mauaji ya silaha yakihusisha wamiliki halali yako juu sana Marekani.
    ingeleta maana km mtoa hoja angeongelea serikali kucontrol watu wanaomiliki silaha visivyo halali hoja ingekuwa na mshiko.

    ReplyDelete
  15. The mdudu,anasema ikumbukwe ndugu zangu ya kwamba MADAWA YA KULEVYA ni HALUBADIRI ya WAHINDI na BUNDUKI ni HALUBADIRI ya WAZUNGU na hivyo vyote mmevipokea kwa mikono miwili sasa mnalalama nn,mjiulize wenyewe kwanza je enzi za Nyerere hayo yote yalikuepo? Kwa upande wangu jibu no na kama yalikuepo na ukatiwa mikononi mwa dola yake basi utakiona cha mote na haijalishi kama ww ni mtanzania au mgeni,mm kwakua naoteshwa nakuona mbali zaidi ndio maana nimesepa mapema na wala sijutii na usepo wangu,

    ReplyDelete
  16. Hhahahahahahaha mdudu kakakuona mzee wa UK umesepa...........haya bwana sema na kiupepo hiko naona kimeshaanza kupulizapuliza anga zetu za Scandinavia huku.

    ReplyDelete
  17. Mchangia mada The Mdudu huoni haya kujisifia kuishi nchi za watu? hebu fanya assessment from the time you left this beautiful country na "ukasepia" huko UK umesha gain nini kikubwa?
    Anyway nyumbani ni nyumbani hata uende wapi patakuwa home kwako na karibu sana pale utakapojisikia kurudi.
    Tanzania ni nzuri na ina fulsa nyingi sana za kutumiwa na ndo maana hata hao Wazungu wanakuja huku na kutajirika sisi tumekuwa brain washed tunaona ujanja kukaa nje.
    Back to our main topic: hata wakati wa Nyerere silaha zilikuwa zinatolewa na zilikuwa zinaingizwa na watu wana miliki kama kawaida hivyo hiyo siyo sheria mpya. Na ikumbukwe wakati wa Nyerere hatukuwa na vyombo vingi vya habari kama ilivyokuwa leo hii ambapo kuna kila aina ya njia ya kupashana habari. Yawezekana wakati huo pia matukio yalikuwepo ila yale magazeti yetu ya MZALENDO na UHURU hayakuweza kuandika kumbuka wakati ule lazima WADAU wachungulie habari kabla haijatoka hahahahahah! Mzee wetu JK Nyerere was a smart dude. Nakukumbusha Saidi Mwamwindi alimuua Kleruu kwa silaha aliyokuwa anaimiliki kihalali kabisa na akamuweka kwenye gari na kumpeleka POLISI mwenyewe na Kleruu alikuwa mkuu wa mkoa na mwanamapinduzi hata Baraka Mwinshehe Mwarukwa alimuimba. Hivyo hata kipindi cha Mwalimu matumizi mabaya ya silaha yalikuwepo sema kulikuwa hakuna njia ya kutoa habari "huru".
    Mimi nadhani cha msingi hapa ni kuboresha taratibu tu na kutoa elimu safi kwa wale wamiliki wa silaha za moto na hilo litasaidia sanaaa.
    Pia restriction ziwekwe kwa umri wa kumiliki silaha ila tatizo wale vigogo wanaowanunulia watoto zao utawadhibiti vipi?
    Kuongezeka kwa idadi ya watu na utandawazi pia vinachangia mambo kama haya. Watu wanaona kwenye MOVIE na hata ONLINE na wanaamua nao kuiga. Wadau hebu nisaidieni kwani kuonesha silaha adharani ni kosa linaloweza kusababishia kunyang'anywa? Mimi nadhani kuonekana nayo siyo mbaya sana, mbaya ni kuitishia pasipokuwa na sababu ya msingi.
    ELIMU NZURI ya matumizi na utunzaji ndo njia pekekee ya kutunasua pia its high time tuanze kuwa na njia sahihi za ku-report matumizi mabaya na POLISI must take immediate action. Kwa nchi za nje suala la kama lililotokea pale ILALA lingekwenda na mkuu wa jeshi la polisi hadi Waziri wake kwa sababu kama tishio lilitolewa polisi na hawakuchukua tahadhali basi moja kwa moja ni " uzembe" na hapo watu wanapaswa kuwajibika.
    The Mdudu nakutakia maisha mema huko ughaibuni, sisi tupo tuna enjoy kula mihogo, viazi na maharagwe safi kabisa. KARIBU SANA!

    ReplyDelete
  18. Ugaidi wa Westgate ulikabiliwa kwanza na watu binafsi wenye silaha kabla ya polisi. Magaidi wanne walikuwa hawana mtu wa kukabiliana nao isipokuwa wenye silaha kama kina Abdul Haji.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...