Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(mbele katika
Jukwaa) akipokea Saalam ya heshima na Utii kutoka kwa Gadi Maalum ya
Gwaride lililoandaliwa na Wahitimu 72 wa Mafunzo Maalum ya Udereva
katika Chuo cha Magereza cha Ufundi na Udereva Kingolwira, kilichopo
Mkoani Morogoro. Hafla fupi ya ufungaji Mafunzo hayo imefanyika leo
Novemba 1, 2013 katika viwanja vya Kingolwira, Morogoro.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kulia) akikagua
Gadi Maalum ya Gwaride lililoandaliwa Maalum kwa ajili ya Ufungaji
Mafunzo ya Udereva Kozi No. 19 ya Mwaka 2013 ambayo yamefanyika leo
Novemba 1, 2013 katika Chuo cha Magereza cha Ufundi na Udereva
Kingolwira, Mkoani Morogoro.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kushoto)
akikagua moja ya Gari aina Bedford ambalo hutumika kufundishia
Madereva Wanafunzi katika Chuo cha Magereza cha Ufundi na Udereva
kilichopo Kingolwira, Mkoani Morogoro. Mafunzo Maalum ya Udereva
yamefungwa rasmi leo Novemba 1, 2013 na Kamishna Jenerali wa Magereza
Nchini.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja akimkabidhi
cheti mmoja wa Wahitimu wa Kozi ya Udereva, Cpl. Nuru kutoka Chuo cha
Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salaam. Cpl. Nuru ni minongoni mwa
askari 11 wa Kike ambao wamehitimu mafunzo Maalum ya Udereva leo Novemba
1, 2013 na Mafunzo hayo yamefanyika kwa muda wa Mwezi mmoja katika
Chuo cha Ufundi na Udereva Kingolwira, Mkoani Morogoro ambapo jumla ya
Askari 72 wamehitimu Mafunzo hao kwa ustadi mkubwa.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(aliyesimama)
akitoa hotuba fupi ya ufungaji Mafunzo Maalum ya Udereva leo Novemba 1,
2013 katika Chuo cha Magereza cha Ufundi na Udereva Kingolwira, Mkoani
Morogoro.
Baadhi ya Askari wa Jeshi la Magereza ambao wamehitimu Mafunzo Maaalum
ya Udereva katika Chuo cha Magereza cha Ufundi na Udereva Kingolwira,
kilichopo Mkoani Morogoro wakisikiliza hotuba ya Mgeni Rasmi. Mafunzo
hayo Maalum ya Udereva yamefungwa rasmi leo Novemba 1, 2013 na Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(hayupo pichani).
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(katikati
walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Askari wa Kike Wahitimu wa
Mafunzo Maalum ya Udereva(waliosimama) mara baada ya hafla fupi ya
ufungaji Mafunzo Maalum ya Udereva yaliyofanyika Chuo cha Udereva
Kingolwira, Mkoani Morogoro leo Novemba 1, 2013( wa nne toka kulia) ni
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa( wa nne
toka kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Naibu Kamishna wa
Magereza, James Selestine(wa pili toka kushoto) ni Asha Said, Afisa
Tarafa Mikese, Morogoro(wa tatu toka kushoto) ni Diwani wa Kata
Mkambalani, Morogoro Kamishna Msaidizi wa Magereza Mstaafu, Daniel
Shawa. Wengine walioketi ni Bwana Fedha Mkuu wa Jeshi la Magereza,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Gideon Nkana(wa pili kulia) na
wa tatu kulia ni Mkuu wa Chuo cha Ufundi na Udereva Kingolwira,
Kamishna Msaidizi wa Magereza, Osmund Nduguru(Picha zote na Lucas Mboje
wa Jeshi la Magereza).
Duuuh!,
ReplyDeleteHawa ndio Maisraeli watoa roho wa duniani
.Wazee wa Lupango, !
.Wazee wa Mukenge, !
.Wazee wa Kaburini, !
Hilo Lori la Bedford Maafande mmeniacha hoi!
ReplyDeleteAu ndio kubana matumizi?
Au ni vile lina Manual gear?
Au ni la Tambiko?