Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda kesho tarehe 29, Novemba 2013 anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Tovuti Kuu ya Serikali katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Uzinduzi wa Tovuti Kuu hiyo inayopatikana kwa anuani ya www.tanzania.go.tzutahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali,  Wananchi, Wafanyabiashara, Washirika wa Maendeleo, Taasisi zisizo za Serikali na Wawakilishi kutoka vyuo Vikuu. 

Tovuti Kuu hiyo ni mojawapo  ya juhudi za Serikali  katika kuhakikisha kuwa taarifa na huduma zinazotolewa na Serikali zinapatikana na kuwafikia wananchi kwa urahisi,  wakati wowote na mahali popote ndani na nje ya nchi. Tovuti Kuu hiyo pia  ni moja ya mafanikio makubwa katika kutimiza dira ya muda mrefu ya kuwa na dirisha moja linalotoa taarifa na huduma zinazotolewa na Taasisi  za Serikali kwa urahisi.

Taarifa na huduma katika Tovuti Kuu hiyozimegawanywa katika maeneo makuu sita ya ambayo ni Serikali, Wananchi, Taifa letu, biashara, Sekta na Mambo ya Nje inalenga kutoa huduma mbalimbali kama upatikanaji wa nyaraka zote za Serikali, huduma zinazotolewa na Serikali kwa njia ya simu na mtandao, Viwango vya fedha, Hali ya Hewa, na Soko la Hisa.

Huduma nyingine katika Tovuti Kuu hiyo imetengwa katika ukarasa wa Nifanyeje? ambao  unamjengea uwezo mwananchi wa kufahamu taratibu za upatikanaji wa huduma zinazotolewa na taasisi mbali mbali za Serikali kama nifanyeje kupata pasipoti, kibali cha kazi, TIN, Cheti cha kuzaliwa na mikopo ya chuo.

Aidha tovuti hiyo pia inalenga kuziunganisha Tovuti na mifumo ya Taasisi mbali mbali inayotoa taarifa na huduma kwa wananchi na wafanyabiashara katika dirisha moja.

Tovuti Kuu hiyo ilianza kutengenezwa mwaka 2009 na kupatikana kwa anuani ya www.egov.go.tz chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Tovuti hiyo iliboreshwa na kuunganishwa na iliyokuwa Tovuti ya Taifa kwa anuani ya www.tanzania.go.tz mwaka 2012 chini ya Wakala ya Serikali Mtandao.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI (MAELEZO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Habari za kutufurahisha kutoka
    idara ya habari(maelezo)tovuti
    hii nakumbuka ipo miaka mingi
    kama imefanyiwa maboresho zaidi
    ni vizuri kwa kuifahamisha jamii
    maendeleo serikali na sekta zote.
    Mikidadi-Denmark

    ReplyDelete
  2. We mdau Mikidadi hilo jina umelipata wapi? Maana Mikidadi,Mkude,Banzi,Koba,Dendego,Uzigo,From Moro,je ww unatoka Moro?

    ReplyDelete
  3. Naipongeza serikali na wadau wote waliofankisha kupatikana kwa tovuti hii. Ni mwanzo mzuri sana. Wadau wote wajitahidi kuchangia taarifa mbalimbali ili iwe up to date.

    ReplyDelete
  4. Ni vizuri kuona viongozi wetu angalau wanajifunza kutoka katika sehemu mbalimbali wanazotembelea nje ya nchi na ni jambo la kujivunia.

    Haya sasa wananchi kazi kwetu tuitumie tofuti hii.

    Mdau Richard- Barani Ulaya.

    ReplyDelete
  5. Naaam na sasa ndio Serikali inaingia ktk DIJITALI kijumla jumla!

    Ni wakati sasa wananchi kuacha malumbano ,Siasa na mabishano yasiyo na msingi ni vile mnaweza kutuma Maulizo na Hoja zenu moja kwa moja kwenda Serikalini kwa njia ya Mtandao ama Dijitali!!!

    ReplyDelete
  6. Mafisadi wa Idara za Serikali (ILI KUHAKIKISHA MNAENDELEA KUTESA KWA RUSHWA NA KUWEZA MONO KWENDA KINYWANI, wasiwasi wangu msije mkautia kwikwi Mtandao wa Serikali ili mrudi ktk Mfumo wenu wa Kizamani wa Makabrasha na Makaratasi !

    ReplyDelete
  7. Duuu Maendeleo Tanzania sasa tunayashuhudia!

    Mimi nitacheka sana haya Masuala na matumizi ya Mtandao na Dijitali yakipiga hodi ktk Taasisi za Usalama kwa ndugu zetu Maafande.

    Hapo ndio utawasikia:

    1.Afande Koplo Marwa akitoa Amri, HAROOO KRUTA Nasema KIDIJITARI MUGUU UPANDE, MUGUU SAWA, AJUWA NYUMA GEUKA KIDIJITARI!

    2.Afande Insepkta Kyaruzi MIMI NASEMA NIANDARIWE MAFAIRI YOTE KWA NJIA YA DIJITARI NASISITIZA HIRO SHARITI RANGU KWA KUWA KWA SASA NATUMIA LAPUTOPU NA SIO MAKABRASHA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...