Jeneza lenye mwili wa marehemu Dkt.Sengondo Mvungi, likiwasili kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo kwa ajili ya kuagwa
 Jeneza likipelekwa sehemu iliyoandaliwa
 Mashada ya maua na picha ya marehemu
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza kutoka salamu za rambi rambi za serikali wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi,kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Katiba Jaji Joseph Sinde Warionba akiongea machache wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi,kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
 Makamu wa Rais Dkt Gahlib Bilali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Katiba Jaji Joseph Warioba, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Mhe Angela Kairuki na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mhe James Mbatia wakiwa katika shughuli za kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi,kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo. 
Misa wakati wa shughuli hiyo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuagwa mwili huo iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda  akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuagwa mwili huo iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo. 

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. TONGA MPOA MGHOSI, URESHINJIA HEDI, MIMI NI MWANACMM CHINJA NYONGA, LAKINI NILIKUA NAKUZIMIA KWA BUSARA ZAKO, INASIKITISHA SANA KUONA KUA WALIOKATISHA MAISHA YAKO NI WALE WANYONGE WA TAIFA HILI BILA KUJALI ITAKADI ZAO ZA KICHAMA KIDINI NAKADHALIKA NDIO ULIKUA MSATARI WA MBELE KUWATETEA,KAMA WAUAJI HAWA WAMEFANYA HIVYO, KIDINI, KISIASA, KWA KIPATO AU KWA CHUKI BINAFSI WAJUE WAMEFANYA KAZI BURE, TUTAMKUBUKUKA KWA KUENDELEA KUTAFUTA AMANI YA MILELE KATIKA NCHI YETU TAMBARARE YA TANZANIA HATA KAMA NA SISI MTATUKATA KWA MAPANGA, MUNGU AKULAZE PAHALI PEMA PEPONI WAUAJI WAKO UTAKUTANA NAO MBELE YA HAKI, HAPA DUNIANI NI SHERIA, KWA MUNGU NI HAKI, LALA SALAMA ROHO INANIUMA SANA, NAWAPA POLE WANAFAMALIA WOOTE, NA WOOOTE WALIOGUSWA NA MSIBA HUU. NASEMA TENA KALALE KWA AMANI, KAZI UMEFANYA.

    ReplyDelete
  2. hao hao walio mstari wa mbele kuomboleza kutoa speech ndo hao walio mmaliza mvungi but wataua wangapi dunia hii ya sasa unamfanyia mtu mabaya asubuhi afu jion unalipwa so mabadiliko lazima hata wakiuwa wakinyonga kuna watakao baki na watashinda hizo nafsi zilizo filisika kifikra

    ReplyDelete
  3. INAUMA SANA.REST IN PEACE BABA. KAZI KUBWA UMEIFANYA TUTAKUENZI DAIMA.

    ReplyDelete
  4. RIP Dr. Mvungi Tanzania itakukumbuka daima kwa mapenzi yako ya kweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...