Balozi wa China Liu Jieyi ambaye nchi yake ni Rais wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu wa Novemba, akielezea yale yaliyojiri wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Usalama uliofanyika jana alhamisi na kujadili hali ya Jamhuri ya Kidemokrasia. Tamko la Rais wa Baraza ambalo limeridhiwa na wajumbe wote 15 wanaounda Baraza la Usalama, wametoa wito kwa makundi ya waasi katika DRC kuweka chini silaha zao, makundi hayo ni pamoja na kundi la M23. Mbali ya kuweka silaha chini yametakiwa pia kuvunjika. Vivile Baraza hilo pamoja na kutambua kwamba kundi la waasi la M23 limemwaga damu ya wananchi wengi wa DRC pia limepoteza maisha ya walinzi wa amani wanaohudumu katika Misheni ya MONUSCO na kwa sababu hiyo Baraza limerejea wito wake kwamba litaendelea kuunga mkono walinzi wa amani maarufu kama Blue Helmet katika utekelezaji wa majukumu yao.
Home
Unlabelled
MAKUNDI YA WAASI DRC WATAKIWA KUWEKA SILAHA CHINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
UNSC-(United Nations Security Council)
ReplyDeleteBaraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,
Suala lipo hivi, Tanzania imegharimika saaana na vita hii ya Mashariki ya Congo-DRC na utitiri wa Makundi hayo ya kivita yapatayo kama 30 au 40 hivi.
Baadhi ya Makundi Makuu na Matawi yao ambayo mengi yana urafiki na mengine uhasimu baina yao.
1.FDLR:
Maatawi yake ambayo mengine rafiki na mengine mahasimu:
.FDLR-LNU
.FDLR-CND
.FDLR-PNC
.FDLR-Maiso
2.MAI MAI:
Matawi yake ambayo mengine ni rafiki na mengine ni hasimu:
.MAI MAI-Jeshi
.MAI MAI-Simba
.MAI MAI-Masharubu
.MAI MAI-Kidevu
1.Waasi wasainishwe 'Kiapo cha Utii' na kupokonywa silaha, NA WALA SIO MKATABA WA AMANI...KUSIMAMISHA VITA SASA NI AMRI YA UMOJA WA MATAIFA.
2.Mpango wa DRONES (Ndege zisizo kuwa na Marubani) ziwepo ili Waasi watakao kiuka Kiapo cha Utii washugulikiwe vilivyo kwa Maangamizi ya Drones, Mpango uwepo eneo lote la Mashariki ya Congo-DRC.
Kama Marekani imweza kuwatwanga Magaidi kwa DRONES kwa nini UN isiwatwange Waasi wa Vita kwa Drones pia?
3.UN-Brigade za Majeshi ya Tanzania ziendelee kuwepo hapo Mashariki ya Congo-DRC kwa kuwa uchunguzi wa waangalizi wa mambo umeonyesha ya kuwa utitiri wa idadi hiyo kubwa ya Makundi ya Kivita imetokana na mgawanyiko miongoni mwao na hivyo yapo Makundi yana Urafiki na Uadui miongoni mwao.
Mfano hao M-23 pana baadhi ya Makundi hapo juu walikuwa na ushirikiano nayo hivyo ni wazi hata kama M-23 imesha decalere kushindwa Mawakala wao bado wangalipo Msituni wakiendelea na Vita hivyo inatakiwa waangamizwe wooote.
Tuangalie ktk FDLR ni kuwa kwa asili ni ADUI wa M-23 lakini Maadui wa FDLR ni lazima watakuwa ni MARAFIKI WA M-23!, vivyo hivyo MAADUI wa M-23 watakuwa ni MARAFIKI wa FDLR!!!