
Tamasha la Krismas
linaloandaliwa na Kampuni
ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha la
Pasaka kila mwaka linatarajiwa kufanyika Desemba 25 mwaka huu jijini Dar es
Salaam.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo jijini Dar, Mwenyekiti wa
Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa asilimia
nyingine 20 itatumika kulipia ada yatima wanaosoma shule mbalimbali hapa
nchini.“Asilimia 80 ya mapato tutaipeleka kwenye ujenzi wa kituo chetu
cha wasiojiweza tunachotarajia kukijenga Pugu, Dar es Salaam, huwa
hatubahatishi tunapodhamiria jambo letu,” alisema Msama.
Kwa mujibu wa Msama, hivi sasa
wanasubiri hati kutoka Wizara ya Ardhi kuhusiana na umiliki wa eneo hilo na
kwamba suala hilo litakapokamilika ndipo mchakato wa ujenzi utakapoanza na wana
imani jambo hilo halitachukua muda mrefu.
Alieleza kuwa wakati wananzisha
tamasha hilo mwaka 2000 dhamira yao ilikuwa kila mwaka kusaidia wasiojiweza.“Niwashukuru wadau mbalimbali
waliotusaidia kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho na mpaka sasa tuna karibu Sh
milioni 120, ambapo gharama nzima ya ujenzi ni kati ya Sh milioni 800 hadi Sh bilioni
moja utakapokamilika.
“Dhamira yetu ni kuwa na kituo
ambacho kitasaidia Watanzania wa mikoa mbalimbali ambao hawana uwezo katika
masuala ya mavazi, elimu, vyakula na mengine mengi,” alisema Msama. Alieleza kuwa Kamati ya
Maandalizi ya Tamasha la Krismas imeamua lifanyike Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam, Desemba 25 na siku inayofuata watatazama mkoa gani waupe heshima.
Alisema hilo litakuwa tamasha kubwa la nyimbo za kumsifu
Mungu na litakuwa na tofauti kubwa iilinganisha na matamasha mengine yaliyowahi
kuandaliwa na kampuni yake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...