Mratibu wa matembezi hayo Bw, Matukio Chuma akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari (MAELEZO), jijini Dar es Salaam wakati akizindua Matembezi ya Nchi Yangu Wajibu Wangu, yanayo tarajiwa kuanza, Januari 11-2014 kuanzia jijini Dar es Salaam hadi Mkoani Morogoro.
Matenzi hayo ya kilomita (200km), ambayo yatachukua siku kumi 10,lengo la matembezi hayo kuhamasisha kila Mtanzania anaamua kuamua kuchukua hatua ya kujikwamua kimaisha.
Ni changamoto inayotolewa mbele ya Watanzania,kukumbuka maana halisi ya uzalendo kujitoa mhanga kuweza kufanikisha maendeleo yao wenyewe kwa kujishughulisha na kujibidiisha katika Nyanja mbalimbali kwa manufaa ya Taifa,kujitolea kuanzia ngazi ya kaya mpaka taifa,kuacha kulalama tu kuwa serikali haijawafanyia moja ama mbili lakini wao wenyewe kutambua mchango wao kama Watanzania na wajibu wao kama wananchi.
Kubwa zaidi kujivunia nchi iitwayo Tanzania kwa yale mema na adimu yaliyopo na kurekebisha palipo na kasoro kwa moyo mmoja bila kujali itikadi,imani, asili ama mtizamo miongoni mwetu, Tanzania,kwa nini Dar es Salaam mpaka Morogoro.
Dar es Salaam imendelea kuwa kituo kikuu cha shughuli nyingi za kiuchumi,kiserikali na vilevile ni mkoa ulio na watu wengi zaidi Tanzania, ta kribani milioni mbili na nusu (2.5mil) kawa mujibu wa sensa ya watu ya mwaka 2002, wakati Morogoro ina watu wasiofika laki tatu tu, na kwa ukuaji wa asilia 4.39,hii inawakilisha tofauti kubwa sio tu kwa idadi lakini ya ukuaji, upatikanaji wa huduma za msingi za kijamii, ukuaji wa kiuchumi na vilivile hali ya kipato na fursa za iuchumi” alisema Chuma.
Mratibu wa matembezi hayo Bw, Matukio Chuma akiwaonyesha waandshi wa habari vazi litakalotumika kwenye matembezi hayo (kushoto), Mratibu wa matembezi hayo Carren Mgonja.
Waandishi wa habari wakishuhudia uzinduzi huo.
Safi sana.Nathibitisha ushiriki wangu, tafadhali toeni maelekezo ya namna ya kujisajili kupitia hapa hapa kwa michuzi.
ReplyDeleteThe mdudu,Anasema nae atashiliki hatakama yuko mbali coz Tanzania na moro ni kama chakula na mboga so najivunia utanzania wangu popote niendapo najivunia pia na moro yangu,,angalizo kwa wadau wote wa mjomba MICHUZI,The mdudu alizaliwa katika kijiji cha KISOLO, huko moro vijijini,lakini haka kadudu leo hii kapo hapa UINGEREZA jamani kaecheni haka kadudu kapumue kametoka mbali sn,amani na upendo kwenu wadau wote.
ReplyDeleteNCHI YETU KWELI NI WAJIBU WETU, NINAUNGA MKONO KAMPENI HII
ReplyDelete