Mwenyekiti wa chama cha wenye viwanda na wafanyabiashara, viwanda na kilimo Tanzania mkoa wa Iringa TCCI , Lucas Mwakabungu (katikati),akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya utafiti  uliofanywa na Institute of Business Environment Strengtheniing for Tanzania (IMED) kwa kushirikiana na Tanzania Chamber of Commerce,Industries and Agriculture (TCCIA) Mkoa wa Iringa uliofanyika katika ukumbi wa Maktaba ya mkoa mwanzoni mwa wiki.(Picha na Denis Mlowe)
========  =======  =========
Na Denis Mlowe,Iringa.

UTAFITI uliofanywa na Institute of Business Environment Strengtheniing for Tanzania (IMED) kwa kushirikiana na Tanzania Chamber of Commerce,Industries and Agriculture (TCCIA) Mkoa wa Iringa umebaini Tanzania inapoteza mapato zaidi ya shilingi bilioni 174  kwa mwaka kutokana na wakulima kutotumia mizani katika upimaji wa mazao ya mahindi na mpunga.
 Mwenyekiti wa chama cha wenye viwanda na wafanyabiashara, viwanda na kilimo Tanzania mkoa wa Iringa TCCI , Lucas Mwakabungu amebainisha hayo wakati akzungumza na wandishi wa habari katika ukumbi wa Maktaba ya mkoa kuwa utafiti huo kuhusu sheria ya vipimo na mizani wa mwaka  1982 unavyosimamiwa na kutekelezwa na kurudiwa Julai na Septemba mwaka 2013.

 Alisema utafiti huo unaonyesha kwa kiasi gani wakala wa vipimo na mizani unatekeleza sheria hiyo na wafabyabiashara na wakulima wanaifuata na kuitekeleza iadha madhara na matokeo ya kutoifuata sheria hiyo.
Mwakabungu alibainisha kuwa mikoa ya Iringa na Njombe pekee inapoteza ushuru wa mazao (crop Cess) ya mahindi na mpunga zaidi ya shilingi bilioni 2.5 kwa mwaka kutokana na mikoa hiyo kuhusika na kilimo cha mazao hayo. Alisema ushuru wa kodi ya mazao unaopotea kwa mazao ya mahindi na mpunga kwa nchi nzima kwa msimu ni shilingi bilioni 14.8.

 Alisema utafiti uliofanywa na IMED ulichukua sampuli za magunia 43 ya mpunga yaliyopimwa uzito na wakala wa vipimo na mizani (WMA) kati ya magunia 482 yaliyokamatwa na kubainika kuwa uzito halisi wa kila gunia ulikuwa wa wastani wa kilo 42 zaidi ya uzito unaostahili sawa na asilimia 56.

 Aidha alibainisha kuwa uzito wa wastani wa gunia la mahindi lililojazwa kwa ndoo za plastiki lina kilo 36 zaidi ya uzito unaostahili sawa na asilimia 40 kutokana na lumbesa ambayo wakulima wanadidimizwa na wafanyabiashara.
Alisema wakulima wanatumia ndoo za plastiki na lumbesa kwa kuwa kuna upungufu wa mizani na ushuru wa mazao kulipwa kwa gunia badala ya uzito na kutokuwepo kwa vifungishio vinavyokubalika.

Mwakabungu alisema utafiti huo ilibainisha kuwa wakala wa vipimo na mizani(WMA) hawana rasimali fedha za kutosha, vifaa vya kutosha na hawana rasimali watu wa kutosha kuwezesha kuitekeleza sheria hiyo kama inavyotakiwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Haya masuala ya kupiga vita lumbesa hayatakwisha kama wataachiwa Wakala wa vipimo wenyewe. Kilimo kipo nchi nzima, sasa hii Wakala inao watumishi wangapi wa kutosha kuzuia lumbesa nchi nzima? Waliwahi kujaribu kufanya operesheni wakati fulani lakini walizidiwa nguvu. Kwani wakati wanafanya operesheni kusini nyanda za juu, kule kaskazini lumbesa za vitunguu toka Mang'ola zinapitishwa. Mimi nadhani dawa ya kudumu ya tatizo la lumbesa ni kushirikisha Serikali za Mitaa ambapo ndiko yaliko mashamba. Kila kata, tarafa na Wilaya izuie kabisa lumbesa kupita katika maeneo yake. Ikibidi patungwe Sheria ndogo ndogo kwa suala hilo la lumbesa huko kwenye ngazi ya chini kabisa ya taifa. Vijiji, kata, tarafa, n.k. zinakosa mapato kwa kuwa hutoza ushuru kwa kuhesabu magunia ambayo ni makubwa sana badala ya kupima uzito kwa kutumia mizani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...