Jina
langu ni Cosmas Hans Moses(22) na dada yangu anaitwa Aneth Hans Moses(24), kwa
sasa naishi mwanza.. Ninaemtafuta ni Baba yetu mzazi anaitwa Hans Moses
Mwakyusa, zamani alikua anaishi Kiabakari Musoma vijijini na huko ndiko tulikopotezana
mimi nikiwa mdogo kabisa kwa hiyo simfahamu hata nikimuona...
Kwa sasa nasikia
anaishi Kyela Mbeya pia ni mfanya biashara ila cjui anafanya biashara gani.Naomba
msaada wenu ili niweze kuonana tena na baba yangu mzazi mawasiliano yangu ni 0765-684572
DREAD LOCKS!
ReplyDeleteRudisha nywere uasili wake la sivyo una hatari ya kukukana.
ReplyDeleteSiku zote ulikuwa wapi usimtafute?
ReplyDeletewatanzania badala ya kumpa ushauri, nyie ni kukosoa maumbile au vibaya watu wanavyofanya!!
ReplyDeleteAu menda kwa nganga
ReplyDeleteachana na hizo piga kazi, hadi kufikia hapo yeye hajakutafuta huoni kama amewatelekeza.. Fanya mambo yako.
ReplyDeleteJamani tuacheni maneno mabaya na yenye kuashiria unyanya paa.
ReplyDeleteKijana ametoa shida anamtafuta mzazi wake, akaona njia muafaka ni kuja hapa jamvini.
Hivyo ni busara ukamsaidia badala ya kubeza kwa kuwa mazingira yaliyo pelekea yeye kupotezana na mzazi wake ni sehemu ya maisha na maisha hayana njia moja kwa mwelewa analijua hili.
Yeye kijana ana makosa gani kupotezana na mzazi wake akiwa angali na umri mdogo sana, kiasi anavyosema hadi hamfahamu akimwona sasa?
Hivyo tafadhali tuwe na busara kwenye masuala kama hili!
Wadau tuacheni dharau !
ReplyDeleteTusitoe maneno mabovu kwa kuwa bado hayajatufika haya na sisi.
Mnajuaje labda ktk ''chomeka chomekana'' zetu hizi inawezekana ikawa zilimwagika mbegu na wewe yakakufika?
Mdau uliyeuliza alikuwa wapi siku zote asimtafute, yeye ni mtoto, je huyo baba siku zote yuko wapi asitafute wanae? Afadhali mtoto kaamua sasa kumtafuta baba yake kwa sababu zozote zile alizonazo, mzazi aliyepotea ndiye wa kumuuliza kitu kama hicho. Si vizuri kumkatisha mtu tamaa kwa maneno kama hayo, kama huna jambo zuri la kusema au ushauri wenye chembe ya maana basi kaa kimya.
ReplyDeleteMdau wa mwisho una lako jambo. Kila kitu kina wakati wake, na kwa yeye huu ndio wakati muafaka aliopangiwa na Mungu kumtafuta baba yake. Naunga mkono mdau aliesema akate hizo dreads maana uasilia wake unakuwa haupo
ReplyDeletehizo nywele hata kama huyo baba ana hamu na wewe utamdisappoint!
ReplyDeleteKatika hali hiyo lazima mtu akukimbie. UMEKUWA KAMA CHOKORAA bwana! Hebu weka nywele zako vizuri ili uweze kukubalika . Hata kama angekuwa mimi nakukana mpaka mwisho.
ReplyDeleteHahaha Urasta imekuwa majanja Bongo!
ReplyDeleteTena hukohuko kwao dogo mkoani Mbeya Marefa wamekataliwa kuchezesha Mpira jana eti kisa?,,,wakate Rasta zao kwanza!!!