Naibu Waziri wa Maendeleo Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amefungua kikao cha Kujadili Matokeo ya Utafiti wa Hali ya Demokrasia katika ngazi za chini kwa mtizamo wa Kijinsia.

Kikao hicho kimeandaliwa na Kituo cha Demokrasia nchini kwa ushirikiano wa Shirika la Kimataifa la IDEA, na kuvishirikisha Vyama vya siasa, Wizara, Halmashauri na Baadhi ya Taasisi Zisizo za Kiserikali.Kuijadili taarifa hiyo. 

Wakati akifungua kikao Mhe.Ummy amesisisitiza kuwa, Demokrasia kamili haiwezi kupatikana bila ushiriki sawa wa wanaume na wanawake na kuongeza kuwa, Serikali za mitaa ni wadau wakubwa wa kuleta usawa wa demokrasia.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akifungua kikao cha majadiliano ya taarifa juu ya Utafiti Kuhusu Hali ya Demokrasia katika ngazi za chini kwa mtizamo wa kijinsia.
Mwenyekiti wa kikao hicho Mhe. Ibrahimu Lipumba akitoa taarifa za Awali za Matokeo ya Utafiti huo. Mhe.Lipumba amesema Utafiti huo ulihusisha madodoso mia sita(600) kutoka katika Mikoa minane nchini.
Mwakilishi kutoka Shirika la Kimataifa la IDEA ndugu Rumbidzai Kandawasvika Nhundu akielezea matokeo ya Utafiti uliofanywa kwa ushirikiano wa Kituo cha Demokrasia na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Baadhi ya Washiriki wa kikao wakati wa majadiliano.
Baadhi ya Washiriki wa kikao wakati wa majadiliano.
Washiriki wa kikao cha kujadili Matokeo ya Taarifa ya Utafiti wa Hali ya Demokrasia katika ngazi za chini kwa mtizamo wa Kijinsia katika picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...