Uncle Salaam,
Sina uhakika kama ujumbe wangu w amwisho uliupata ukautupa kapuni au hukuupata. Cha msingi ni kuwa sasa ni miezi miwili tangia tupate maji kwa mara ya mwisho na hakuna dalili yeyote ya kupata huduma hiyo kwa hivi karibuni.
Hali zetu ni mbaya sana na tunahitaji msaada wa haraka wa huduma hii ya msingi kwa maisha ya binaadamu; chodechonde kama serikali yetu imeshindwa tunaomba tusaidiwe msaada wa kupata maji hata kutoka nje ya nchi!! Kwa maisha ya mtanzania wa kawaida hatutaweza kuendelea kununua bidhaa hii kwa muda mrefu, na teyari tunaanza kuona vijana wakichota maji kwenye madimbwi na kuuza.
 
Chakusikitisha zaidi hakuna sehemu yeyote ya kuomba msaada tukasikilizwa, tunakuomba utuwekee ujumbe huu hewani huenda tukapata wasamaria wema kama si hapa nchini basi hata nje ya nchi.
 
Hali ni mbaya sana huku kwa Ali maua.
Mdau Muathirika

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hili eneo kwa kweli hali ya upatikanaji wa maji ni mbaya sana, na hisi meneja wa Dawasco wa kanda hii hajui anachokifanya maana sidhani kama anataarifa kamili ya eneo Zima analoshughulikia. Mtu mmoja anasababisha wananchi waone serikali nzima haifanyi kazi yake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...