Mhe. Naibu Waziri wa Maji, Dk. Binilith Mahenge ameendelea na ziara yake mkoani Dodoma katika kangalia utekelezaji wa miradi ya maji ya vijiji 10 katika Halmashauri hiyo kupitia mpango wake wa Big Results Now.
Dk. Mahenge ametembelea miradi mbali mbali ikiwemo Ng’humbi, Kibaigwa, Ntomoko na Mkoka na kujionea maendeleo ya miradi hiyo hadi kufikia sasa.
Dk. Mahenge ametembelea wilaya za Mpwapwa, Kongwa na Kondoa na anategemea kumaliza ziara yake leo Jumamosi.
. Mhe. NWMA, Dk. Binilith Mahenge akiwa
katika chanzo cha maji,
Ng’humbi.
Mhe. NWMA, Dk. Binilith Mahenge akiwa
katika harakati za kukagua
tanki la mradi wa maji wa Mkoka.
Mhe. NWMA, Dk. Binilith Mahenge akisikiliza
maelezo akiwa juu ya tanki la kuhifadhi maji, mradi wa maji Ng’humbi.
Dk. Binilith Mahenge akiwa kwenye mradi
wa maji Kibaigwa.
Heko Dr. Bilinith Mahenge!
ReplyDeleteAma kweli mzigo mkubwa abebeshwe Mnyamwezi!
Ndio uzuri wa kumpa kazi mtu kulingana na Fani yake.
Dakitari anawajibika yeye mwenyewe kuhakikisha kama kazi imetendeka vyema!!!