Mnamo April 18, mwaka huu mamlaka ya viwanja vya ndege (TAA) ilisaini mkataba wa dola za kimarekani 168 (takriban bilioni 275 za Kitanzania) na kampuni ya BAM International ya Uholanzi kwa ajili ya ujenzi wa awamu ya kwanza ya Terminal III ya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Ujenzi wa awamu hiyo ya kwanza unaotarajiwa kuanza karibuni ukikamilika terminal hiyo itakuwa na uwezo wa kuhudumua abiria milioni 3.5, ambapo awamu yake ya pili ililamilika itakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 6, na itakuwa ni kwa huduma ya ndege za kimataifa. Sehemu iliyopo sasa ya uwanja huo, yaani terminal II, itatumika kwa abiruia wa ndani.
Haya ndiyo mambo tunayotaka, ukienda airport za wengine unatembea ndani kwa ndani mpaka unachoka unataka uje nyumbani ukute vitu vinavyoeleweka kama hivi. Ni taswira nzuri.
ReplyDeleteitachukua siku chche tu kabla hatujauchafua na kuacha kila kitu kikininginia na ac kutofanya kazi.
ReplyDeletePoor Design.Nina wasiwasi kama wadau hasa Tanzania Airport Authority walishirikishwa kutoa maoni wakitaka terminal mpya iweje.Ukiangalia kwenye hii michoro mfano inaonekana bado gate ni moja moja.Sasa hiyo B747 imepaki na watu wote wanaboard kupitia gate moja hamuoni kwamba ni uzamani ? wanaongelea kuweza kuhudumia A380 .kwa hizo gate moja moja ? Guys you are not seriuos
ReplyDeleteNarudi tena uncle . Hivi terminal yenyewe ina gates 5 ina maana ndege tano tu kwa wakati.hivi waliopanga mchoro wanaangalia expansion mmekwenda hata jomo kenyatta mkaona wana ngapi ? muunganiko na terminal 2 ukoje .I hope hii information haikutoka TAA kwa maana kwamba sio ramani final kwani hamna msala
ReplyDeletetunapo focus kuwa structure itakayohudumia watu in 50 yrs to come or more inabidi tuwe na design inayoendana na kipindi hicho, sioni km hii design itatupeleka ktk kipindi hicho, labda kama in btn tutabomoa na kujenga tena upya, majengo hayana mvuto ni kama mabohari ya kuhifadhia nafaka...tatizo lipo wapi jamani? Hatuwezi kuwa na ka structure kama ka Oliver Tambo SA?
ReplyDeleteInabidi tubadilike tukikabidhiwa tuutunze kwa kuweka bajeti za matengenezo au kuwapa kandarasi kampuni mbali mbali za usafi, umememe, matengenezo-mabomba. Ushindani uliopo sasa hivi kila mahali utusaidie kuboresha kila kazi na huduma inayotolewa kwa manufaa ya Abiria na sisi wenyewe.
ReplyDeletemmmh let me be positive. Congrats
ReplyDeletekwanini waweke abiria tofauti abbiria wandani uwanja wao,wanje uwanja wao sasa hapo ndio nini uwanja wenyewe mbaya hautoshi chochote maduka hakuna yaani sipendi watu kulipua kazi fanye kwa akili jamani.
ReplyDeleteMdau wa mwisho nakuunga mkono, let me be positive too. Congratulations Tanzania. Wamejitahidi jamani hatuwezi kufanya kila kitu kizuri kwa wakati mmoja taratibu tutafika huko mnakowaza. Wenzetu walianza hivihivi na wamefika hapo walipo. nafikiri tutafika tu. Polepole ndio mwendo. Mungu ibariki Tanzania
ReplyDeleteJamani. Mimi wa Isabako Sengerema nashangaa tu, eti ni seme nini na hata kituo cha daladala ni chini ya Mbuyu, Ah tutafika.
ReplyDeleteTuapange mambo IKIWEPO UWEZO USAFIRISHAJI KWA IDADI YA ABIARIA WA VITU KAMA VIWANJA VYA NDEGE NAVINGINEVYO tukizingatia vifuatavyo:
ReplyDelete(i)TANZANIA POPULATION GROWTH,
(ii)EMERGING WORLD TRAVEL NEEDS,
(iii)ECONOMIC GROWTH AMBAYO ITA-ATRACT TRAVEL DEMANDS KUBWA ZAIDI.
Kama mnavyoona mali zinazopatikana GAS, OIL, MINERALS zitavuta idadi kubwa ya wahamiaji HALALI NA HARAMU kama tulivyo shuhudia wimbi la mamilioni ya Hahamiaji waliobebwa na Opersheni Kimbunga, hiyo ni Trela mchezo bado unakuja watajazana tena zaidi ya wali fukuzwa nchini.
Population growth rate ya Tanzania ilikuwa 2.8% mwaka 2002 na mwaka 2012 ikashuka kidogo ikawa 2.6%
SENSA NA IDADI YA WATU KWA MIAKA:
-Mwaka 1961 watu 7.5 Milioni
-Mwaka 1978 watu 28.0 Milioni
-Mwaka 1988 watu 35.0 Milioni
-Mwaka 2002 watu 39.0 Milioni
-Mwaka 2012 watu 44.9 Milioni
Pia mwaka 2030 Tanzania inakadiriwa kuwa na watu 51.00 Milioni !
SASA KWA KASI HIYO YA ONGEZEKO LA IDADI YA WATU TANZANIA NADHANI UWANJA WA NDEGE WA KUBEBA KWA MWAKA ABIRIA 6 MILIONI HAUTOSHI !!!
kiongozi uliyekuja na statistics za idadi ya watu umemaliza kila kitu,WaTZ hatuendi na statistics tunapofikiria kuweka mambo makubwa, mfano stand kuu ya mabasi zamani ilikuwa Kisutu na Mnazi mmoja, ikahamishwa na kuwekwa ubungo kwani ilionekana ubungo panatosha, leo hii nasikia wanaihamishia nje kabisa ya Mbezi, ni jambo jema, lkn je kwanini kipindi kile hatukuwaza kuwa na structure kubwa Mbezi ambayo tungefocus kwa kipindi kirefu mfano 30-50 years?....
ReplyDelete