Msichana akiwa amevalia nguo zenye rangi ya bendera za Tanzania, akiwa ni mmoja wa vijana wengi wanaoonesha mavazi ya kila nchi mwanachama wa Jumuiya ya Madola wakati wa kikao cha CHOGM 2013 hapa Colombo, Sri Lanka. Wadau wengi waliomuona wamefurahi sana na kushauri kamati iliyopewa kazi ya kubuni vazi la Taifa wamwangalie msichana huyu pia katika kufikia muafaka. Alichovaa msichana huyu ni sare ama sari ya Sri Lanka yenye bendera ya Taifa letu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Vazi la Taifa kwa Tanzania:

    Hivi hatubuni la kwetu mpaka tuone huko nje ya nchi mtu amevaa ndio tuje ku-kopi na ku-paste?

    Huu ni Utumwa gani wajameni wa kila kuiga kila kitu?

    Muziki tunaiga!

    Mavazi tunaiga!

    Tabia tunaiga!

    Kwa nini kwa suala la Vazi la Taifa tusingeanzia palepale kwenye MGOLOLE weu ama RUBEGA na tukurupukie kuona msichana mevaa huko Sri Lanka?

    Tanzania tuwe tunajitegemea na kujiamini kwa mambo yetu!!!

    ReplyDelete
  2. Ehhh Wjameni!

    Tanzania tueacha Rubega na Mgolole huku tukiwa huko Sri Lanka tunarikia Mavazi ya Kihindi ndio yawe vazi la Taifa?

    ReplyDelete
  3. Wazo la Kukopi hilo vazi nakataa!

    Tuwe na Mipango ya VAZI LA TAIFA inayo jitegema kawa Watanzania!

    ReplyDelete
  4. Watanzania tuna MAJANGA haya Mawili hapa chini:

    1.Tuna KANSA mbaya sana ya kuto thamini vya kwetu.

    -Je, wale Wataalamu wetu wa Sanaa akiwemo Ndg. Rasta Merinyo na wengine waliishia wapi ktk mchakato wa vazi la Taifa?

    2.Tuna UTUMWA wa kiakili wa kuto kujiamini na vya kwetu na kuona ya kuwa vya wenzetu ndio bora zaidi!.

    -Utaona idadi kubwa ya wenyeji Wakonongo wa Kitanzania ktk Migahawa ambayo inaandaa vyakula Bandia 'JUNK FOODS' kama vya Majuu., Wakati Wageni waelewa wana viepuka na kwenda Masokoni kununua vyakula asilia vikiwa vibichi kutoka Mashambani!!!

    Sasa Majanga hayo mawili KANSA ya kuto kuthamini vya kwetu na UTUMWA wa kiakili ndio vinajiri watu kupendekeza tuige vazi la Sri-Lanka kuwa la Taifa la Tanzania!

    ReplyDelete
  5. Hapa tupo pamoja mia kwa mia,au vazi la kike la kimasai linawapendeza sn kina mama zetu na madadazetu,,hakika nchi nyingi zingeyakubali hayo mavazi,,na hao waliopewa jukumu la kutafuta vazi la taifa,,mbona wako na mwendo wa jongoo,,ndio maana mm sitaki kuludi huko coz idala zote mwendo wa konokono wezenu huku mwendo chui au chita,,WARUGULU tuna msemo unaosema KALEGENI BAHO,,ni mm yuleyule ndugu yenu THE MDUDU K,

    ReplyDelete
  6. mmeshasema sari ya sri lanka iweje tena vazi la taifa? au hata nikivaa skin tight ina rangi za bendera tayari ni vazi la taifa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...