Diwani wa Kata ya Isongole Ndugu Gwalusako Kapesa akielezea namna gani wananchi wa ilaya ya Ileje wamechoshwa na taratibu za serikali za kuwalazimisha kununua mbolea za ruzuku za Minjingu kwani zimekuwa hazina faida kwao kama wakulima na zimewaletea hasara kubwa sana, wananchi hao wameiomba serikali na viongozi wake kuwasikiliza zaidi wao katika kutatua kero zao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Kalembo na kuwaambia kilio cha wakulima kinafanana karibia nchi nzima hasa kuhusu matatizo ya mbolea na kusema CCM itachukua hatua kwa kukutana na waziri husika kwenye kamati kuu itakayofanyika mapema mwezi ujao.
Wananchi wa Kata ya Kalembo wakiwa wamejifunika miamvuli kujikinga na mvua wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake ambao upo ziarani mkoani Mbeya.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...