Habari iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde toka jijini Arusha,inaeleza kuwa Ndege ya abiria aina ya Boeing 767 ya shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines) mchana huu imeshindwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutoka na hitilafu iliyokuwepo Uwanjani hapo na kulazimika kutua kwa dharula kwenye Uwanja wa Mdogo wa Arusha.
Wataalam wa Ndege wapo eneo la tukio hivi sasa kutafakari namna watakavyoweza kuwashusha abiria hao na kutafuta namna ya kuweka sawa mambo ili Ndege hiyo iweze kuruka.
Ndege hiyo ilikuwa na abiria zaidi ya 200 na wafanyakazi 9. kabla ya kupaa tena ilibidi abiria wote wateremke, na kupunguzwa mafuta ili kupunguza uzito wa ndege hiyo. Abiria waliamuriwa kwenda kupandia ndege hiyo kwenye Uwanja wa Ndege wa KIA.
Globu ya Jamii inaendelea kufatilia kwa ukaribu tukio hilo,na tutaendelea kufahamishana kadri taarifa zitakavyokuwa zikitufikia.
Mjomba sio boeing 787 ni boeing 767-383ER
ReplyDeleteKuna watu lazima wawajibishwe kwenye hili. Kwann wasi clear runaway na badala yake kuidirect ndege kubwa kwenye uwanja mdogo. Itarukaje ss?
ReplyDeleteni aibu sana kwa nchi yetu. Ni hitilafu gani hizo zilitokea uwanjani? Kuwepo miundombinu mibiovu Tanzania ni Matokeo ya ufisadi!
ReplyDeleteEbu tuacha siasa,Rubaoteni alitakuwa kuwa na mafuta ya ziada yatakayo mwezesha yeye na ndege yake kutua kiwanja kinachoweza kuhudumia hiyo aina ya ndege yake, Endapo kukatokea dharula yoyote, Iyo ndege iliyokuwa kwenye Runway aikokotwi kama magari au baiskeli, kuna taratibu za kufanyika hapo. Pongezi kwa Rubani kwa kuweza kunusuru uhai wa abiria wote hayo mengine ni makosa ya kibinadamu...
ReplyDeleteHii ndege ni kubwa sana....kwa kutua kwa dharura Arusha bila kupoteza maisha ya Abiria ni jambo nzuri...ila sasa kiuchumi inatuharibia
ReplyDeleteumasiki wa mawazo ni moja ya tatizo kubwa kuliko yote,kazi za kupeana ndiyo madhara yake,
ReplyDeletemsilalamike airlines wakikata safari za kuja bongo. kwa mwendo huu kama mimi ningekuwa investor ningekata safari za ndege zangu. hii inadamage reputation ya brand yako kwa customers.
ReplyDeleteNimeona gari za zimamoto kwanza nikacheka hahahahaha wamekimbilia utadhani wana maji ya kutosha....yaani pale wameshukuru kweli...Bongo bwana tunasonga kibahati bahati tu.
ReplyDeleteNashauri kabla hujaandika mtafutage ushauri wa watu wanaojua aviation :
ReplyDelete1.Gari la kusukuma ndege halipo KIA wala Arusha airport.Lazima litoke Nairobi au Dar
2.Kwa case hiyo ndege lazima itolewe na Boeing test pilots tu na si vinginevyo.Pia itafunguliwa viti vyote ,watoe mizigo yote
3.Ukishadeclare fuel emergency lazima uchanguzi ufanyike.ikibainika kwamba ulikuwa na mafuta machache kama walivyofanya hawa jamaa , marubani wananyang'anywa leseni na hata hilo shirika kufungiwa kutua nchini
kwa hiyo nakataa hayo maelezo kwamba abiria walielekezwa kwenda kupandia ndege hiyo KIA.ungesema walielekezwa kwenda kupanda ndege nyingine KIA
sio kazi tu hata vyeti vya kupeana Hivi hawa waongozaji ndege pale airport wanasoma wapi. Lakini kwani kama kuna hitilafu airport si ndege inazunguka baandae inaruhusiwa kutua. Sasa mnaanza kutoa mbaya bila ya kujua taratibu za uongozaji ndege.
ReplyDeleteWabongo ni wababaishaji tu. Lazima makosa yatakuwa yametokana na uzembe wa wabongo. Haya sasa image ya nchi inapotea, watalii wanaweza wasije tena maana usafiri utakuwa wa shida kama ndege zitakataa kutua KIA. SHAME ON YOU wababaishaji wa Tz.
ReplyDeletePongezi kwa rubano,ila Nachojiuliza ni jinsi gani Ndege hiyo itakavyoondoka uwanjani hapo,cause kwa taarifa ni kwamba uwanja una 1.1mile while ili ndege hiyo iweze kupaa inahitaji Njia ya urefu Wa 2.5 miles.
ReplyDeleteEthiopian Airlines booking Grab cheap Ethiopian airlines flight tickets, pay less - save more. No hidden charges.
ReplyDeleteEthiopian Airlines booking Grab cheap Ethiopian airlines flight tickets, pay less - save more. No hidden charges.
ReplyDeleteEthiopian Airlines booking Grab cheap Ethiopian airlines flight tickets, pay less - save more. No hidden charges.
ReplyDelete