Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani Ulaya Ngoma Africa aka "FFU Ughaibuni",
inawatakia kila la heri na fanaka waTanzania wote kwa kuadhimisha miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania (bara),Uongozi wa bendi hiyo unaiombea kila la heri, Serikali ya Tanzania,Wananchi na Taifa la Tanzania
Ngoma Africa band inawaombea wadau na wananchi wote popote walipo kutumia wakati huu kujikomboa kimawazo, na kuhakikisha kuwa tunajenga na kudumisha amani, umoja, mshikamano na upendo wa kitaifa, ili kuleta maana kamili ya Uhuru wa maisha ya Mtanzania.
Katika Kusherehekea miaka 52 ya Uhuru, watanzania tunapaswa zaidi kujenga na kuziba nyufa zinazo bobomoa au kujaribu kubomomoa msingi wetu imara wa umoja,Upendo na mshikamano wa kitaifa.
Mungu Ibaraki Tanzania !
Mungu wabariki Watanzania !
Mungu Ibariki Serikali ya Tanzania !
Tafadhali pata burudani kamili at www.ngoma-africa.com
Miaka 52 iliyopita kulikuwa hakuna nchi inayoitwa Tanzania bara!
ReplyDelete