WaTanzania Evans Mhando (L) na Fatuma Matulanga (M) walipokutana jijini Beijing nchini China. Wiki hii walikuwa wageni katika kipindi cha HUYU NA YULE kinachotayarishwa na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production
Katika huyu na yule wiki hii, nimepata nafasi ya kuzungumza na vijawa wawili wa kiTanzania wanaosoma nchini China. Nao ni Fatuma Matulanga aliyeko Beijing na Evans Mhando aliyeko Nanchang ambao kwa pamoja tumejadili mambo kadhaa na zaidi kuhusu vijana
Wameeleza mengi wakioanisha kijana na maisha ya China na Tanzania ikiwemo
1: TOFAUTI KATI YA KIJANA WA CHINA NA TANZANIA
2:TOFAUTI KATI YA ELIMU YA CHINA NA KWINGINE. Ni kweli kuwa China haifunzi ubunifu na ndio maana wanasifika kwa kuendeleza kuliko kubuni?
3: MALALAMIKO KUWA BIDHAA ZA CHINA HAZINA UBORA, YANATAZAMWA VIPI HUKO CHINA?
4: NI KIPI WANACHOJUA SASA KUHUSU CHINA AMBACHO HAWAKUJUA KABLA HAWAKWENDA CHINA?
5: MABADILIKO YA SERA YA MTOTO MMOJA MNAONA IMEPOKELEWA VIPI HAPO?
6: NI KIPI WANACHOTAMANI KINGETOKA CHINA KWENDA TANZANIA (HASA KATIKA TASNIA YA HABARI?)
Na mengine mengi

Ni huyu na Yule ya Mubelwa Bandio wa Jamii Production akihojiana na Fatuma Matulanga na Evans Mhando, wanahabari wa shirika la utangazaji la Tanzania (TBC) wanaojiendeleza kielimu nchini China
Kwa maoni ama ushauri, usisite kutuandikia kupitia jamiiproduction@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...