Chuo cha Diplomasia katika kuendeleza wito na wajibu wa kutoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu, wiki iliyopita kilifanya kozi fupi ya Utatuzi wa Migogoro na Usuruhishi yaani CONFLICT RESOLUTION AND MEDIATION,kwa siku mbili mfululizo (tarehe 11-15 nov 2013).

Hivyo basi washiriki mbali mbali toka sekta binafsi na mabenki nchini,bila kuisahau Sekta ya Umma walishiriki kama Mkuu wa Wilaya ya Temeka, Mh. Sophia Mjema

Wawezeshaji wa Mafunzo haya ya muda mfupi kawaida huwa ni mabalozi na wakufunzi waliobobea sana katika mambo ya Diplomasia hivyo kuwapa washiriki uzoefu na kesi halisi zilizowahi kutokea katika eneo husika la mafunzo ili kuwajengea uwezo na waweze kwenda kufanyia kazi moja kwa moja mafunzo na utaalam walioupata.
Mkuu wa Idara ya Utafiti, Uchapishaji, Ushauri na Kozi fupi, Bwana Juma M. Kanuwa akisisitiza jambo wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo, na akasema kuwa mafunzo yanayofuata ni ya Itifaki na Mahusiano ya Umma yaan PROTOCOL AND PUBLIC RELATIONS.
Mafunzo hayo yakiendelea kutolewa.
washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa wawezeshaji Balozi C. A. Sanga ( aliye katikati na amevaa kaunda suti) kushoto kwa Balozi ni Bwana Alex Ngusaru toka CRDB plc (mwenye suti nyeusi) na anayefuatia ni Mama Sophia Mjema, Muu wa wilaya ya Temeke wakiwa na washiriki wengine (attached Picture name is: CFR with Amb. Sanga, C.A)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...