Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.
KAMPUNI ya Megatrade Investiment Ltd ya jijini Arusha imekabidhi
zawadi katika kituo cha kulelea watoto yatima na waishio katika
mazingira magumu cha Kili Center kwa ajili ya msimu wa siku kuu za
mwisho wa mwaka.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zwadi hizo meneja mauzo na masoko wa
Megatrade Goodluck Kway alisema msaada huo ni sehemu ya faida
iliyopatikana kutokana na utumiaji wa kinywaji cha K-Vant Gin hivyo
kampuni ikaonelea ni vyema ikarejesha kwa jamii hususani watoto
waishio katika mazingira magumu.
Alisema Mega trade investment ltd imetoa zawadi ya kilogram 50 za
mchele, kilogram 100 za Unga wa Sembe,kilogramu 50 za unga wa
ngano.kilogramu 75 sukari na kwa ajili ya kupikia lita 50.
Vitu vingine ni Katoni mbili za sabuni za kufulia,Dawa za meno,Mafuta
ya kupaka mwilini,Vinywaji vya aina tofauti sanjari na madaftari kwa
ajili ya maandalizi ya mwaka mwingine wa masomo utakao anza January
mwakani .
“Megatrade tunatambua kuwa watoto yatima pia wanayo haki ya
kusherehekea siku kuu za Krismas na mwaka mpya kama walivyo watoto
wenzao na ndio sababu tumekuwa na utaratibu wa kuwapatia msaada kila
mara pindi tunapo pata nafasi”alisema Kway.
Aliziomba taasisi nyingine na makampuni mbalimbali kujitokeza
kulisaidia kundi hilo ambalo hivi sasa linakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa vifaa vya shule hususani kwa watoto
wanao bahatika kuendelea na masomo.
Akizungumza kwa niaba ya watoto wenzake Neema Omary aliishukuru
kampuni ya Megatrade kwa kuwakumbuka kwa msaada huo huku wakiendelea
kutoa wito kwa watu binafsi na makampuni mengine kujitokeza kutoa
msaada ambao utawasaidia katika shughuli zao mablimbali za
kimaendeleo.
Meneja mauzo wa kampuni ya Megatrade ya jijini Arusha Goodluck Kway (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watoto waishio kwenye mazingira
magumu wa kituo cha Kili center cha mjini Moshi kabla ya kukabidhi
zawadi kwa ajili ya siku kuu za mwisho wa mwaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...