Naibu Waziri wa mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Mhe. January Makamba akiwa na mkewe Ramona Makamba wakipokewa na Afisa Ubalozi Mindi Kasiga(wapili toka kushoka) na mwenyekiti wa Vijimambo Baraka Daudi mara tu walipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia. Mhe. Makamba amekuja maalum kama mgeni rasmi kwenye sherehe ya Uhuru wa Tanzania itakayofanyika Jumamosi Desemba 7, 2013 Laurel, Maryland nchini Marekani.
Afisa Ubalozi Mindi Kasiga akimweleza jambo Mhe. January Makamba wakati alipokwenda kumpokea uwanja wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia.
Mheshimiwa Naibu Waziri wa  Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwenye picha ya pamoja na Makatibu Wakuu na Maafisa wa Ubalozi. Kutoka kushoto ni Bw. Paul Mwafongo (Kaimu Balozi), Bw. George Yambesi (Katibu Mkuu Utumishi), Mhe. January Makamba, Bw. Peter Ilomo (Katibu Mkuu Ikulu), Bw. Suleiman Saleh (Kaimu Mkuu wa Utawala).
Mhe. January Makamba Picha ya pamoja na  Ujumbe wa PSPF wakiwemo maafisa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
 Mhe. January Makamba na mkewe Ramona wakibadilishana mawili matatu na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mindi Kasiga.
 Kutoka kushoto ni Afisa Ubalozi Abbas Missana, Afisa Ubalozi Mindi Kasiga, Ramona Makamba na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Mhe. January Makamba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kumbe muheshimiwa January ameoa? Siku jua ila nimefurahi kumuona mama . God bless

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...