Taarifa ya mkutano wa wanachama wa chama cha mapinduzi wa maeneo ya District of Colombia, Maryland na Virginia ( DMV)
 Tunaombwa kwa umoja wetu kuhudhuria mkutano wa wanachama wote ili kujadili mambo mbalimbali yanayohusu kuimarisha tawi letu.Pia fomu za kugombea nafasi ya wajumbe 10 wa halmashauri kuu ya tawi, katibu UWT, katibu Wazazi na Mwenyekiti umoja wa vijana zinapatikana, tafadhali wasiliana na viongozi ili upewe maramoja ujaze na kuziwakilisha kabla ya mkutano. Tunawakaribisha  wote wanaotaka kujiunga na CCM uandikishwaji wa wanachama wapya utakuwepo siku ya mkutano.
Tafadhali usikose kuhudhuria ili sauti yako isikike na ushiriki kikamilifu kukijenga chama chetu na kuleta maendeleo ya nchi yetu.
MAHALI:  1400 University Boulevard Langley Park, Maryland 20783                        ( TABEER RESTAURANT)
SIKU:          Jumapili, DECEMBER 15,   2013
SAA:           5.00 p.m -8 pm
1.     Taarifa fupi ya Tawi
2.     Mikakati juu ya uimarishaji wa tawi letu
                                    3.   Uchaguzi wa viongozi wa tawi( NAFASI ZILIZOWAZI)
                           4.  Mengineyo

Tafadhali tujitokeze kwa wingi kama ilivyo desturi yetu kina Baba tunaomba maji na soda na kina Mama Vitafunio. Tafadhali zingatia muda.
Asanteni

                                                            Uongozi wa  CCM Tawi la DMV

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Na sisi wana Republican Party tutakuwa na mkutano wetu hapo Buguruni kwa Malapa siku hiyo. Wote mankaribishwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...