Kuna dada anaitwa HAPPYNESS KASIL anautafuta ukoo wa mama yake mzazi kwani haufahamu.
Mama na baba yake wote ni kabila la wasukuma,mama yake amezaliwa NGUNDU wilaya ya NKWIMBA mkoa wa MWANZA.Baba yake amezaliwa NYANGUGE –BARIADI –SHINYANGA.
Mama yake anaitwa MATHAR DANIEL.Baba yake anaitwa KASIL SANAGU MAJAB.Mama yake alifariki mwaka 2001.Baba yake pia alifariki mwaka 2010.Katika familia yao walizaliwa watoto sita
1.Charle Kasil
2.Happyness Kasil
3.Faustn Kasil
4.Daniel Kasil
5.Mariam Kasil
6.Neema Kasil
Wamefariki watoto 3 na wamebaki 3 .Waliofariki ni Charle Kasil ,Mariam Kasil na Neema kasil.Waliobaki ni Happy kasil. Faustn kasil na Daniel Kasil.Wazazi wake walikuwa wanaishi NYARUGUSU GEITA –MWANZA.
Baba yake alikuwa akinunua dhahabu Nyarugusu na anauza MWANZA.Mama yake alikuwa mama wa nyumbani.Mama yake alisoma shule ya sekondari NGUNDU wilaya ya NKWIMBA mkoa wa MWANZA na kuhitimu form 4.Anamfahamu mama yake mkubwa anaitwa ESTHER DANIEL alikuwa anaishi MWANZA sasa hivi hafaamu alipo .Shangazi zake ni SALOME SANAG na LUSIA SANAG.
Salome alikuwa anaishi MSOMA na Lusia alikuwa anaishi NGULYAT.Bibi na babu mzaa baba walikuwa wanaishi NYANGUGE BARIADI.Jina la ukoo wa baba yake ni SANAGU MAJAB.Kwa sasa Happy na wadogo zake wanaishi SIRARI9mpakani mwa Tanzania na Kenya) .
Anaomba mtu yoyote anae ujua ukoo wa mama yake amjulishe kwa namba zifuatazo (+255 782 781834)
MDAU WA GLOBU YA JAMII
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...