Mwanamke wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 amekutwa na kilo 1.1 za madawa ya kulevya aina ya heroin alizokuwa amezihifadhi tumboni mwake,baada ya kukamatwa huko Macao, nchini China. Dawa hizo zenye jumla ya vidonge 66 vinakadiriwa kuwa na thamani ya dola za Kimarekani 137,720.
Mwanamke huyo alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne iliyopita. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko Chima.
Pichani ni mwanamke huyo wa Kitanzania (akiwa amefunikwa uso) aliyekamatwa na kilo 1.1 za heroin huko Macau. Hapo amepigwa picha na vidonge vyake wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Macau, Disemba 19, 2013.
ReplyDeletewewe muandishi macau na china vitu viwili tofauti kabisaaa macau is a part of hongkong and not china
rekebisha sema MACAU,HONG KONG
alafu huyo mwanamke ni mjinga maana siku hizi ukiwa umetoka BKK kuingia HKG lazima upigwa xray pole yake
Macau na HK ni nchi moja ya China mwandishi yupo sawa, sema hizo sehemu mbili ni majimbo huru chini ya China. Yanajitegemea kwenye ulinzi na mambo ya nje. Vile vile yote yalikuwa chini ya ukoloni wa ureno(macau) na HK(uingereza). Na ndo mana China wana sheria ya kunyonga Kwa kusafirisha unga wakati sehemu huru wana sheria zao tofauti.
DeleteAjari kazini!Jasho litamtoka china!
ReplyDeleteNdio mambo safari hii amebambwa. Kama angevuka basi ni millionea akirudi Bongo. Je Macau wana sheria ya kunyonga?
ReplyDeleteMie napenda kweli wakishikwa. Sema hii nchi hawanyongi, wangewanyonga tu yaishe, hajaanza leo wala jana, kujiringisha na mapicha ya cl na brand bags, wenyewe wanaita no fake zone, kumbe kazi ni kuuwa wenzae. My uncle was a drugg addict alikuwa anatuibia mpaka vijiko ili apate hela ya unga, mkifua inabidi mlinde kwa kupokezana maana keshaiba sana nguo ili apate hela ya unga.
ReplyDeleteHuyu dada ni full maonyesho na alishawahi kuulizwa kama anauza unga akijibu kuwa ye ni mzuri hawezi uza unga, leo kiko wapi full kandambili badala ya CL.
Wanatuchafua sana sasa hivi kila tunakopita tunanuka.
Mungu wangu!
ReplyDeleteOhhh haya maisha ya juu bila Mipango ya maana kwa ndugu zetu akina dada wa Kitanzania yatafanya wasichana wooote warembo kuishia Magerezani nje ya nchi!!!
Hapo katika hizo US Dola 137,720 utakuta yeye Punda hata US Dola 10,000 ni tabu kulipwa kama Mshahara wake na huyo Bosi wake aliyemtuma !
ReplyDeleteshe has sealed her fate, death by firing squad, how sad!
ReplyDeleteYa nini tabu?
ReplyDeleteYa nini kuchezea Kifungo Kirefu Gerezani ama kuhukumiwa Kifo?
Isiwe tabu, Tanzania ina Fursa nyingi mno za kuyapata Mapesa ni kufunguka kiakili utaziona !
1.Kilimo cha Kisasa,
2.Biashara ya Madini,
3.Ujasiriamali wa kawaida,
4.Huduma za Kibiashara ikiwemo Lishe na mengineyo,
5.Mauwa na Urembo,
6.Mazao ya Maliasili,
7.Uwakala wa Huduma
-Vocha za Simu za Jumla
-Maji na Bidhaa za Vyakula vya Viwandani (Bakhresa, Metl, n.k)
FURSA HIZO 7 HAPO JUU KWA UCHACHE WAGENI HARAMU WANAINGIA TANZANIA NA KUZICHANGAMKIA HADI Mhe.RAISI KIKWETE ANAWATIMUA NA OPERESHENI KIMBUNGA!
JAMANI KAMA WAO WAMEWEZA WANA NINI, NA SISI TUKISHINDWA TUNA NINI?
WAKATI NCHI NI YETU NA FURSA NI ZETU HADI TUKAUZE MADAWA UGENINI NA KUTUGHARIMU KIFO AMA KIFUNGO KIREFU?
Ohhh masikini weee ndugu yetu!
ReplyDeleteAmesema ngoja nijaribu kidogo haka kamzigo ka Kilo moja na GrAMU 100 labda nitafanikiwa MATOKEO YAKE SASA ANACHUNGULIA KABURI!!!
Maisha ya juu yanaponza!
ReplyDeleteIli kubakia kukaa juu siku zote wanalazimika kuuza Madawa ya kulevya.
Heri mimi nimeridhika na Dona langu kwa dagaa chungu la Kigoma kwa akina Diamond Plutnumz!!!
Jamani katika ni hivi,
ReplyDelete1.Michezoni kwenye Usajili wa Ligi kuna Usajili Mkuu na pia Dirisha Dogo la Usajili!,
2.Maisha pia kama ilivyokuwa Michezo yana Plan-A na pia Plan-B, kama Plan-A inakuwa ngumu ni vema kuchukua Plan-B!
Tuachane na maisha ya kutaka mafanikio makubwa na kwa haraka, twende mwendo wa Pole Mwenyezi ni Tajiri sana atatupa tu!
Tusije kwisha kwa kunyongwa Ugenini maana nchi zingine sio kama kwetu pana Mipango mipango huko hata Hongo hakuna ukishikwa ni Kisu kooni tu!
Tuangalie Mipango mbadala ya kufikia malengo ya kimaisha na tuachane na kasi ya kuifukuza Sarafu!!!
WATU HAWAKOMI!! KUNA WA WATU KIBAO DAR NA WAKE ZAO WANAJENGA MAJUMBA KWA BIASHARA HII WAKIDHANI NDIO MAISHA MAZURI. SINA HURUMA KABISA NA WATU HAWA.
ReplyDeletewapenda njia za mkato. Na shule labda walikuwa wanataka maksi bila kusoma.
ReplyDeleteunajuwa hiyo ni njia ya mkato kwenda kaburini, jamaa sheria yao ni kifo.
Masikini weee Dadetu alijipigia mahesabu yake hiyo tarehe 19 Disemba, 2013 anamaliza Mazagazaga ya biashara yake MKWANJA KIBAO MKONONI US$ 137,170 KUZITIA KIBINDONI kutoka kwa hao macho madogo (China) halafu ile tarehe 24 Disemba , 2013 mchana wa mapema anatua nyumbani Dar-Bongo kuja kuanza Mkesha wa Krismasi!
ReplyDeleteHaikuwa hivyo, dadetu anajikuta KRISMASI mwanawane yupo CHINA tena LUPANGO !
Why are so growing to give up our freedom for money, very disappointing!!!!
ReplyDeleteMajanga!, jamani majanga!
ReplyDeleteDada yetu anapigania mpango wake tena tarehe za Krismasi ili achane zake bata baada ya kupata Fwedha, ohhh anajikuta pwaaa chini ya Ulinzi China anavikwa Ninja Jeusi kichwani na Pingu mikononi !,,,Kizibiti ubaoni na Wanalibeneke hewani mapicha kwacha kwacha bila chenga live.
Ama kweli mwaka wa balaa 2013 namna hii unaisha kwa msala?
Tujikhalifu nafsi zetu kwa kuanza maisha mapya kwa kazi za Kuchoma maandazi na vitumbua na kunaanga mihogo!
ReplyDeleteMasuala ya Biashara hizi za Madawa tutakwisha, Mchina ananyonga sana hata Umoja wa Mataifa na Amnesty International wameilalamikia sana, lakini wapi msimamo wao upo pale pale KISU, BASTOLA , KITANZI!
Maana Viwanja vya ndege dunaini vimekuwa vigumu hakupitiki kabisaa tutanyongewa ndugu zetu sana !
Mchangiaji wa kwanza hapo juu, Unakosoa kumbe unakosea. Mwaandishi alichokiandika ni sahihi na kwa taarifa yako Hong Kong na Macau zopte ni mamlaka ya China ni sehemu ya Jamhuri ya watu wa China. Macau ilitawaliwa na wareno na Hong Kong na waingereza. Zote mbili zimerudishwa katika mamlaka ya China ambayo inaendelea pia kuidai Taiwan.
ReplyDeletedemu mwenyewe mbona kama mzungu tena
ReplyDeleteUnderstandably mdau wa 20 amekasirika sana but hamna haja ya matusi. I m surprised ndugu Michuzi has published the comments. Anyway, whatever the punishment this woman is going to get is not enough. Madawa haya yanaharibu watoto wa watu. It destroys families. It kills people be it Tanzanians or otherwise. Can u imagine how this womans ndugu feels? Inawezekana ana katoto pia. Masikini ya Mungu. Jamani tamaa ni mbaya. Utajiri wa haraka haraka hauna baraka. We have a beautiful fertile country. Use it to make a healthy living please... message to those who have same plans as this unfortunate woman.
ReplyDelete