KAMPUNI ya Tan Communication media imetoa misaada ya chakula yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki mbili kupitia kampeni ya Ushindi kwa ajili ya kuwafariji watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi katika vituo kumi jijini Arusha.
Akizungumza wakati wa chakula cha pamoja cha mchana jana Meneja mbunifu wa kampuni hiyo Vicky Mwakoyo alisema kuwa lengo ni kuwafariji watoto hao ambao jamii ya watanzania imewasahau.
Mwakoyo alisema kuwa watanzania wanatakiwa kubadilika na kuwajali watoto yatima ikiwa ni pamoja na kutenga muda wao kukaa na kucheza nao ikiwa ni pamoja na kuwapatia zawadi mbalimbali ili wasijione kama ni wapweke na wameachwa peke yao.
“Watoto wote ni sawa na watoto hawa hawajapenda ni mapenzi ya Mungu hivyo tunawajibu wa kutenga muda wetu na kukaa na watoto hawa kama hivi leo unaona wamefurahi kama watoto wengine wenye wazazi”alisema Mwakoyo
Aidha aliongeza kuwa ni vyema jamii ikajenga utamaduni wa kuwasaidia watoto hawa na isiishie misimu ya kipindi cha sikukuu tu kwa kuwa wanamahitaji ya chakula kila siku.
“Naomba niiombe serikali kupitia Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto kuangalia namna ambavyo inaweza kushirikiana na vituo vya kulelea watoto yatima kwa kuwapatia fungu ili kupunguza ukali wa maisha katika vituo hivyo kwa kuwa vina mchango mkubwa kwa taifa”alisema meneja huyo
Tukio hilo liliofanyika katika viwanja vya Matongee Carnivo limewakutanisha watoto Yatima zaidi ya Mia moja na hamsini ambapo walipata nafasi ya kushiriki michezo mbalimbali kama kuvuta kamba,kukimbia kwenye magunia,mashindano ya kula na kuimba muziki.
Vituo hivyo vilivyopatiwa misaada ni pamoja na Bethlehemu,Moshono Foundation,Tumain,Mama na Watoto,St.Joseph,Camp Mosses,Kambarage Lemara na Karama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...