Wadau,
Nipenda kuwataarifu kwamba maandalizi ya ule mpambano wa kumaliza mwaka 2013 kati ya Wahenga Veterans na Golden Bush Veterans yamekamilika na game itachezwa uwanja wa TP al-maarufu Nangwanda Sijaona. Mechi itaanza saa kumi na nusu, yaani masaa matatu yajayo.
Hivi sasa Golden Bush Veterans tunapanda chakula cha mchana kwa pamoja hapa Star Light Hotel, na tunategemea kuanza msafara mrefu kuelekea uwanjani kuanzia saa tisa na nusu. Msafara utanzia start light Hotel hadi uwanja wa St James Park “Kinesi” ambapo tutasimama kwa muda ili kupata maelekezo kutoka kwa kamati yetu ya Ufundi na Mambo ya Kale jinsi ya kuingia uwanjani. Kazi hiyo itafanywa na mwenyekiti wa kamati bwana Jeremiah Mulungu ambaye ndiye atakuwa mkuu wa msafara kuanzia St James Park hadi Nangwanda Sijaona.
Huwezi amini mpaka hivi sasa uwanja wa TP umefulika watazamaji wa kila aina, watoto, vijana, wazee kila mmoja akiwa na hamu kabisa ya kuona mtanange huu wa kukata na shoka. Ikumbukwe kwamba Wahenga walishinda mechi kama mwaka jana, hivyo Golden bush wanaingia kwa ajili ya kulipa kisasi.
Baada ya game timu zote mbili pamoja na jamaa na marafiki zetu waalikwa, tutajumuika pamoja ili kufanya tafakari ya jinsi tulivyomaliza mwaka 2013.
Nichukue nafasi hii kuwakaribisha wapenzi na wakereketwa wa soka, waje waone football ya hali ya juu sana ambayo itachezeshwa na Mwamuzi anaetambuliwa na FIFA.
Karibuni sana.
Ticotico
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...