Baadhi ya wahitimu wa
mafunzo ya awali ya ukocha waliokabidhiwa vyeti vya kozi hiyo wakiwa katika
picha ya pamoja na vyeti vyao. (picha zote na Denis Mlowe).
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya awali ya ukocha waliokabidhiwa vyeti vya kozi hiyo kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa shule ya kimataifa ya Southern Highland Kitova Mungai.
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Wilaya ya Mufindi Gervas Choga akimkabidhi cheti ya kozi ya awali ya ukocha Lupyana Massawe, kulia ni mkurugenzi wa Hazina Foundation William Mungai makabidhiano yaliyofanyika katika ukumbi wa John's Corner mjini Mafinga.
========== ========= ===========
WAKABIDHIWA VYETI VYA
UKOCHA WA AWALI
Na Denis Mlowe,
Mufindi
ASASI isiyo ya
Kiserikali ya Hazina Foundation iliyoko Mafinga imekabidhi vyeti 26 kwa
wahitimu wa kozi ya awali ya ukocha kwa walimu wa Shule za Msingi na Sekondari
wa Wilaya ya Mufindi.
Akikabidhi vyeti hivyo
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Wilaya ya Mufindi Gervas Choga aliwataka wahitimu
hao kwenda kuvumbua vipaji vilivyojificha mashuleni na kuwaendeleza soka katika
wilaya ya Mufindi.
Alisema mafunzo
waliyopata ni muhimu sana kwa maendeleo ya soka la wilaya ya hiyo na taifa kwa
ujumla na serikali inatakiwa kuwekeza katika michezo na kuondokana
na siasa iliyotawala sasa kwa watu wengi kujiingiza katika mpira kwa lengo la
kupata umaarufu na mwisho kujiunga katika siasa.
Choga alisema vipaji
vya soka vinaanzia shule za msingi hivyo ni jukumu la kila mmoja wenu kuweza
kuandaa michezo ya kila mara katika shule mnazofundisha na maeneo
yanayowazunguka.
“Nitahakikisha kila
mmoja wenu anayafanyia kazi mafunzo haya na hakuna hata mmoja nisiyemjua hivyi
katibu nakuagiza wafatilie wahitimu hawa na kuona wanafanya jambi kuhusu soka
la wilaya yetu linakuwa, naomba vijana mtusaidie katika kuendeleza soka kwa
kupitia mafunzo mliyopata” alisema Choga
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Hazina Foundation,William Mungai aliwataka wahitimu kuyatendea
haki mafunzo hayo kwa kuwafundisha watoto mpira wa kisasa kuweza kufikia
malengo ya kukuza soka la Mufindi na Taifa kwa ujumla.
Wiliam Mungai alisema
mafunzo ya ukocha yatakuwa endelevu kwa walimu na wadau mbalimbali watakohitaji
kujifunza ukocha ngazi ya awali na asasi ya Hazina itagharamia mafunzo hayo kwa
vijana wa wilaya hiyo.
Alisema mafunzo hayo
yanatakiwa kuanzia ngazi ya chini na bila kubagua jinsia kwa kufundisha
vijana wenye uwezo n kuthamini mpira wa miguu kunakuwa na faida kubwa na
manufaa kwa vizazi vijavyo
Wiliam Mungai iliitaka
serikali kuwekeza katika vyuo vyingi vya ufundishaji michezo kwa faida ya miaka
ijayo katika kukuza michezo na kuongeza pato la Taifa.
“Naomba sana vijana
wangu mwende mkafundishe soka la kisasa kwa vijana wetu nategemea sana kila
mwaka kuongezeka kwa vipaji katika wilaya yetu na msiishie hapa na kozi hii ya
awali mjiendeleze katika fani yenu na kama mnavyojua soka la
Tanzania kwa sasa lipo nyuma sana so tuanzie huku chini kwa kuibua vipaji vya
kutosha” alisema Willam Mungai.
Mafunzo hayo
yalioendeshwa na Kocha Bonifas Mkwasa mwezi Juni 25 hadi Julai 6 mwaka
huu kwa udhamini mkubwa wa asasi ya hazina Foundation inayomilikiwa na Wiliam
Mungai na makao makuu yako mjini Mafinga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...