Salamaleko Ankal na timu yako nzima ya Globu ya Jamii,

Naomba unisaidie kushea na Wadau Dukuduku langu hili,nililokumbana nalo leo baada ya kutoka duka la dawa Maeneo ya msikiti wa Wangazija na hospitali ya Hindu Mandal baada ya kukuta kukuta gari langu limetiwa pingu kama. 

Tukio hilo limetokea mapeka leo pale nilipoegesha gari nje ya duka hilo na kuingia ndani kwa ajili ya kununua dawa baada ya Krismas nzima kuwa mahututi kwa mguu kuvimba,niliegesha gari katika eneo wazi ambapo hakuna kibao chochote kinachoonyesha ishara ya HAKUNA KUPAKI GARI HAPA na mbele niliona kuna gari la serikali limepaki hapo nami nikapaki nyuma yake.

 Lakini cha kushangaza kama si kustaajabisha,ni pale nilipotoka dukani na kukuta gari langu limefungwa na na kukutana na Vijana wa Tambaza Auction Mart wakinitaka nilipe faini ya laki moja. 

Nilipowauliza kuwa mbona hakuna kibao cha No Parking na hajanizuia wakati naegesha gari na huku mkiniona wakati naingia pharmacy tena kwa kuchechemea, vijana hao hakutaka kuelewa somo lolote zaidi ya kuniambia niende Anatoglo nikalipe faini halafu nije kuchukua gari langu. 

Kiukweli haki haitendeki juu ya swala hili linaloendelea hapa mjini,maana imekuwa kama ni mradi wa mtu wa kutafuta hela kwa nguvu,maana haiwezekani sehemu haina alama yeyote na watu wanakuona hawaji kukutaarfu kuwa sehemu hii haipaswi kuegeshwa gari na labda kaegeshe eneo lile,lakini hawa jamaa wanakutegea umeegesha halafu na wao wanakuja na machuma yao na kufunga gari.

Kitu cha pili kwa akili ya kawaida tu mtu anaonekana ni mgonjwa na hawezi kutembea na hajazuia mtu hamwezi mkatoa ushauri? 

Halmashauri ya Ilala mnapaswa kufanya utaratibu mzuri wa kuwafanya hao Tambaza Auction wakusanye hela na watoe uthibitisho kama wafanyavyo polisi . Hii kwenda hadi Anatoglo kulipa faini kisha ndio urudi kuchukua gari lao ni sawa na ucheleweshwaji unaofanywa na STRABAG Ubungo. 

Meya wa Ilala Jerry Silaa angalia usumbufu huu unapoteza masaa mengi ya uzalishaji.

Mdau aliekumbwa na Mkasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. kweli hao tambaza pia wanafanya utapeli. nilifungwa siku Moja kufika anatoglo wanakupunguzia faini kutoka hiyo laki muja hadi elf 70 lakini 50 unapewa risit Na 20 ni rushwa. mbaua zaidivwatasingizia Umeme Hamna Wa kutoa copy ili uache hiyo risiti, waendelee kudanganyia watu.

    ReplyDelete
  2. Salamaleko ndo nini?

    ReplyDelete
  3. sheria nzima ya nani ana haki ya kuruhusu au kutoruhusu magari kuegeshwa sehemu yeyote Tanzania nzima inahitaji kuangaliwa na serikali kuu haraka sana.

    Imekuwa siku hizi ni mradi kwa kila mtu mwenye biashara utadhani wao ndio wamiliki wa maeneo wanayofanya biashara.

    ReplyDelete
  4. mdau unalalamika nn?hayo ndio matokeo ya rushwa ambayo watendaji (maybe ukiwamo wewe) mmeilea hadi ilipofika...maana watu wanadhani wakila rushwa maofisini na ufisadi wa kutisha kwa kutumia peni & nyadhifa zao hali hiyo inashia juu kwa juu tu..NO WAY watu wa chini nao wanawaona na waiga tena kuwapita!

    ...tena mdau walipoona hilo gari kubwa four wheel wakajua ndio fisadi mkubwa huyu so atupunguzie chenji za ufisadi anaoufanya..si umeona mwenzio hapo ana terios wamemwacha!!pole sana!

    itafika mahala nchi itakuwa chungu sana hata kwa wenye pesa kama tatizo la ufisadi halitashghulikiwa kutoka juu

    mdau uk

    ReplyDelete
  5. Mdau uliekumbwa na mkasa. pole sana. huu ni kukosa ustaarabu sana, pamoja na hao vijana, kama kweli wametumwa kufanya hivyo, kwa maelezo yako naona basi wanafanya kazi kama robot!
    hata miji mikubwa kama Qunu, Tokyo, J'burg, NYC, Boston, LA hakuna faini ya namna hiyo! Upuuzi sana!
    Mdau anaeikasirikia nji yetu kwa haya maupuuzi ya kishenzi

    ReplyDelete
  6. Traffic laws ziko clear, law enforcers wanatakiwa wawe responsible na mtumiaji barabara unatakiw auwe responsible, kama hakuna kibao kinachosema "No Parking", basi wapeleke mahakamani na wakulipe pesa yako na ya usumbufu pia, tena usipate shida, kesi yako (which is straight forward) mpe mwanasheria, ili waje kulipa gharama zote

    ReplyDelete
  7. Pole sana mdau.Next time ukipark Mazingira kama hayo,na kwa muda mfupi, chukua TRIANGLE ZAKO MBILI weka mbele na nyuma ya gari lako au washa taa za HAZARD,hawatalifunga gari lako(May be)!.Suala la Alama(sign boards) liangaliwe kwa sababu "No news is good news"-Jiji lijitahidi kuweka alama zaa NO PARKING mahali ambapo halitaki watu waegeshe magari.

    David V

    ReplyDelete
  8. Hawa jamaa hata maana ya parking hawajui.
    Mimi walikama gari nikawambia wapi inaonesha no parking jibu lao hairuhusiwi kuegesha upande wa kulia.
    Nika hoji wapi alama inayoonesha hivyo imewekwa, kwanzia katika alama za barabarani mpaka katika vitabu vya Road Safety and Security,
    Wakabaki kulazimisha faini.
    Ikanibidi kuelekea kwa Mwanasheria wa Wilaya wa ILALA na mkurugenzi wa Biashara wa Ilala kwa ufanuzi zaidi.
    Nikamtafuta na mtu anayehusika na barabara naye kwa ufanuzi.
    Mwisho nikawambia hawa jamaa wa TAMBAZA naombeni muniandikie makosa yangu katika form husika kwa sababu siwezi kulipa ninaelekea MAHAKAMANI, kwa sababu nilipata uthibitisho wote kutoka mahala usika kuwa wapo katika makosa.
    Majibu yao Muachieni huyu jamaa atatuaribia kazi.

    Hawa ni waizi kabisa...
    Kwa nini hilo la SERIKALI hawajalifunga kufuli kama sio wizi.

    ReplyDelete
  9. Wana hasira ya kukosa mapato kwa siku mbili nzima za holidays.

    ReplyDelete
  10. Lipa pesa, Acha malalamiko kwanza angalia jinsi julivyo park gani lako

    ReplyDelete
  11. Inaelekea umepark kwa makosa, kwani kuna magari mawili hapo kushoto wame parki inavyotakiwa,. lakini wewe umepark jeep lako kama wewe unavyotaka na hivyo wewe kuoccupy nafasi 2 au 3 za parking.Basi kama ndiyo hivyo basi una kosa la kupark gari lako vibaya na hapo alama NO PARKING haitakiwi iwepo.point iliyoko hapo wewe waulize alama ya kuonyesha jinsi ya kupark magari au mistari iliyochorwa chini(Parking lines)

    ReplyDelete
  12. Salamaleko ndio nini sasa

    ReplyDelete
  13. POLE SANA MDAU ULIYEPATA MATATIZO HAYA NA KUSHARE NA SISI. MIMI YALINITOKEA SIKU YA TAREHE 24.12 2013 NA NILIKUWA DUKA LA DAWA. HAKUNA NO PARKING, WATU WENGINE WENGI WAMEPARK TU BILA WASIWASI. SASA NILIENDELEA NA UTARATIBU HUO NIONE NINI HASA KINAENDELEA. WALITAKA NIWAPE HELA NIKA KATAA NIKAAMUA NILIPIE. HAPO NDIO ILIKUWA SHIDA. ILA NILISHANGAA KUONA KUWA FINE YA MANISPAA NI TSHS 50,000 NA YA KWAO NI 50,000. SIJUI BUNGE GANI LIMEPITISHA. KWA KWELI KAMA UNAWEZA WASILIANA NA MH. JERRY
    mdau Bongo

    ReplyDelete
  14. Mdau @UK kwa kweli philosopher yako ni ya hali ya juu sana. sasa inabidi kuwaaelimisha watu waelewe ili tubadilishe serikali. kaka hali ni mbaya sana hapa nchini. kama huhongi unakufaaaaa. ukisikia shehena imekamatwa na polisi..ukweli ni kuwa wameshindwana kukubaliana hongo. the Athari tutaiona miaka michache ijayo.

    kama kuna mtu anaweza saidia tunaomba msaada.

    ReplyDelete
  15. Kwa mwendo huo kweli tutafika? Bongo bwana. Mungu tusaidie

    ReplyDelete
  16. I would not be surprised that the Govt are aware of these clampers. They are necessary evils. They control the parking system otherwise watu wanapark magari ovyo ovyo na it makes the city look untidy. All i can advise my fellow Tanzanians is communicate with people and find out if it is ok to park there. But i also think the city council should have signs put up to alert drivers of parking zones, and fees etc. As one mdau hapo juu states no news is good news. I say better safe then sorry, so ask around before parking.

    ReplyDelete
  17. Inasikitisha kuishi ktk nchi ambayo mtu anaweza kujiwekea sheria mwenyewe zikaweza kuwakandamiza wengine na hakuna wakuwakemea.What's point kuwa na government isiyojua waangalia watu wake. I think don't pay and waripot police kwani wanachokifanya ni kinyuem cha sharia.

    ReplyDelete
  18. Sasa kwanini huku mpigia simu boss wako akalipa hiyo laki moja faster faster? Next time usiwaletee pozi watoto wa mjini. As far as I know that road parallel park is not possible.

    ReplyDelete
  19. KWA KIFUPI TUUU NI KWAMBA UKIWA MTOKA N'JE YAANI MKAZI WA ULAYA AU USA NA KWINGINEKO NA UNAJUWA HAKI ZAKO ZA MSINGI KIMATAIFA USISUMBUKE KUFIKIRIA SANA SHERIA ZA TANZANIA MAANA ZIMEWEKWA KWA WASIOJUWA HAKI ZAO. NYIE NDUGU ZETU MLIEKO N'JE TETEYENI URAIYA MARA MBILI YAANI UWEPO UWEZEKANO WA MTU KUMILIKI PASSPORT MBILI AU TATU, ILI UKOMBOZI WA NCHI HII UPATIKANE MAANA NIMEONA KWENYE COMMENTS NYINGI WACHANGIAJI NI WAKAAJI WA N'JE, SASA TELEMKENI MRUDI KUKOMBOWA NCHI. HAPA BONGO AKIJA ASKARI AKAKUTISHA TISHA UKIOGOPA UMEMPA NAFASI YA KUKUTOWA CHOCHOTE LAKINI UKIDINDA UTAMUONA ANAISHIA KWA KUJIKOSHA ETI UNAJIFANYA MJANJA UTAKIONA CHA MOTO. LAKINI NDIO IMETOKA HIVYOOOO. KWA SISI WENYEJI TUMESHA YAZOWEA HAYO MAISHA TUANAYAONA YA KAWAIDA.

    ReplyDelete
  20. Ni halali yako kulipa. Maana uli-park vibaya sana. Angalia wenzako walivyokuwa wame-park. Nafasi ya magari matatu; wa-park wewe peke yako?? ULITEGEMEA NINI? Ni halali kufungwa.

    ReplyDelete
  21. Anon hapo juu tuanzie kugombania uraiya mara sita ili sheria ikishtuka watatugawia angalau nusu
    yaani uraiya mara tatu au mara nne hata tano au sita ikiwezekana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...