Meneja Habari na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Promosheni yao mpya kupitia Bia ya Castle Lite  ya kupata washindi 12 watakaokwenda nchini Afrika Kusini kushuhudia onyesho kubwa la msanii maarufu duniani,Timothy Zachery Mosley kwa jina Maarufu anafahamika kama TIMBERLAND,Promosheni hiyo itaendeshwa kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia leo Januari 20 mpaka Machi 30.Kulia ni Meneja wa Bia ya Castle Lite,Victoria Kimaro.
Meneja wa Bia ya Castle Lite,Victoria Kimaro akisisitiza jambo juu ya namna wateja wa bia hiyo watakavyoweza kushiri kwenye Promosheni hiyo,ambapo amesema mteja atatakiwa kununua bia hiyo ya chupa na atakapoifungua ataona namba zilizowekwa ndani ya kizibo na atatakiwa kutuma jina lake na namba hiyo kupitia ujumbe mfupi wa simu kwenda kwenye namba 15499.
Meneja wa Bia ya Castle Lite,Victoria Kimaro akionyesha namba itakayokuwa inatumika kwenye Promosheni hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...