Pichani ni Uongozi wa juu wa  Chama cha Wasanii wa Filamu hapa nchini.a.k.a Bongo Muvi,kulia ni Katibu Mkuu,William Mtitu,Mwenyekiti,Steven Mengere a.k.a Steve Nyerere,Katibu Msaidizi Bi.Devotha Mbaga,Mweka hazina Mkuu, Issa Mussa Cloud pamoja na Makamu Mwenyekiti ,Mahsein Awadh maarufu kama Dk Cheni wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuchaguliwa hapo jana na wadau mbalimbali wa tasnia hiyo waliokutana kwenye viwanja vya Lidaz club,jijini Dar.
Pichani ni Mwenyekiti wa chama cha Wasanii wa Filamu nchini a.k.a Bongo Muvi, Steve Mengele ‘Nyerere’ akizungumza mara baada ya kuchagulia kushika wadhifa huo wa Uenyekiti,Steve alisema kuwa atahakikisha haki inatendeka kwa kila msanii wa filamu,kuhakikisha kipato kinaongezeka katika tasnia yao,kama vile haitoshi alieleza kuwa atakutana wasambazaji wote wa filamu kuzungumza mikakati mbalimali ya kuhakikisha tasnia hiyo wasanii wake wananufaika na  kazi zao na kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.Steve anashika nafasi hiyo ya Uenyekiti iliokuwa imeachwa wazi na Msanii Vincent Kigosi a.k.a Ray.
“Tatizo kubwa kwa wasanii wa Bongo Movie hawajitambui kama wao ni watu wakubwa. Wanajiuza kirahisi kwa wasambazaji wakati karibu kila nyumba ya Mtanzania haukosi filamu moja ya Bongo Movie,” Aliongeza Nyerere ambaye pia anafahamika kwa jina la ‘Kata simu’.
“Wasanii wa Bongo Movie tunadhulumiwa kwa sababu hatutambui haki zetu. Leo wasanii watatu wanakwenda Mwanza wanapewa shilingi milioni mbili, Diamond peke yake anapewa shilingi milioni 15,”alisema Nyerere
.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii wa Filamu,Dk Cheni akiwashukuru wadau mbalimbali waliotoa ushirikiano mkubwa kwa namna moja ama nyingine kuhakikisha uchaguzi wa viongozi katika tasnia hiyo wanapatikana,ikiwa ni shemu ya kuhakikisha maendeleo yanazidi kupatikana ndani ya chama hicho
Katibu Mkuu wa Chama cha Wasanii wa Filamu a.k.a Bongo Muvi,William Mtitu akizungumza machache na kuwashukuru Wanachama na wadau mbalimbali katika suala zima la kufanikisha kuwachagua viongozi wawatakao,ambao watahakikisha chama chao kinasimama imara.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii wa Filamu nchini a.k.a Bongo Muvi,Vincent Kigosi a.k.a Ray akitoa shukurani kwa wanachama na wadau wa tasnia yao waliofika kwenye uchaguzi huo,Ray amewataka viongozi hao wapya kuendelea kuijenga tasnia hiyo katika suala zima la kuhakikisha inaendelea kukua siku hadi siku.
Ray akifafanua jambo kwa ufasaha mara baada ya kukabidhi nafasi yake ya Uenyekiti kwa mwenyekiti mpya Steve Nyerere.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Ndugu wawili waliovaa suit jackets ingawaje wamependeza lakini wananitoa raha. Can people dress appropriate to weather conditions please? Joto sana bongo sasa hivi ni lakutisha. The guys must feel rather uncomfortable and less focused. Umaridadi before comfort is not advisable.

    ReplyDelete
  2. mdau 1-1

    Hawa Film-Stars wetu wa bongo
    wapo mazingira ya Air-Condition wakimaliza wanaingia kwenye gari yenye AC hakuna tatizo hapa la kuwalaumu mavazi badala kusifu wametokelezea. Tatizo la wewe kutokwa na raha ni joto au mavazi?
    mikidadi-Denmark

    ReplyDelete
  3. Hakuna shida, hapo ni full AC

    ReplyDelete
  4. Jamani hawa ndugu zangu wanasafari ndefu sana kwa jinsi tasnia ilivyo na haya mazingira ya kufanyia uchaguzi bado naona swala la umakini hafifu kwenye hii fani wachache watatoka na wengine watabaki kubeba majina tu.Hongereni kwa uchaguzi but umakini muhimu sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...