Meneja wa kituo cha Redio Nuru Fm, Victor Chakudika cha mkoani Iringa akimkabidhi Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa wa Iringa Rustica Tung'ombe moja ya viti vinavyotumiwa na walemavu , makabidhiano hayo yalifanyika katika hospitali hiyo mwishoni mwa wiki.'
baadhi ya viti vya walemavu na fimbo za kutembelea vilivyotolewa na redio Nuru Fm ya mkoani Iringa kwa hospitali ya rufaa mkoa wa Iringa(picha na Denis Mlowe).
Baadhi ya Wafanyakazi wa Nuru FM wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Iringa
========= ======= ==========
HOSPITALI YA RUFAA IRINGA YAPATIWA VIFAA
Na Denis Mlowe,Iringa
SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Iringa Development of Youth Disabled and Children care (IDYDC) kwa kushirikiana na Redio Nuru Fm ya mjini Iringa wametoa misaada ya viti 5 vya kubebea wagonjwa na fimbo 20 za kutembelea kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 3.5
Sambamba na kuisadia hospitali hiyo radio hiyo ilivisaidia vituo vya watoto ya yatima vilivyoko mkoani hapa vya Huruma Center,Sabasaba Center na kituo cha wazee Iringa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula, vifaa vya usafi, sabuni na mipira kwa watoto hao.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo wakati wakitimiza miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa kituo hicho, meneja wa radio Victor Chakudika,aliitaka jamii kuwa na moyo wa kujitolea kwa jamii inayoishi katika mazingira magumu kwa lengo la kuisaidia serikali majukumu ambayo wadau wenye uwezo wanaweza kuyatatua.
Alisema lengo la redio kuwa jirani na jamii inayowahudumia katika kuwapatia matangazo yao ya kila siku hivyo misaada iliyotolewa ni kurudisha faida kwa jamii hiyo na itakuwa inafanyika kila mwaka kwa kutoa misaada kwa wanaohitaji hasa kwa wanaoishi katika mazingira magumu na vituo mbalimbli vya afya vilivyoko mkoani hapa.
Chakudika alisema radio hiyo inatambua umuhimu wa kuchangia huduma za afya, kwani bila wananchi husika kutokuwa na afya njema ina maana hata maendeleo hayatakuwepo hivyo ni wajibu wao kwa kusaidiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha sekta ya afya inafanya kazi ipasavyo na kuwahudumia watu wote kwa usawa.
Kwa upande wake Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali hiyo Rustica Tung’ombe kwa niaba ya Mganga mkuu aliishukuru radio hiyo kwa kujali na kuthamini maisha ya Watanzania, kwa kuamini kuwa mchango huo si tu ni kusaidia shughuli za hospitali bali pia utasaidia kuongeza viti katika hospitali hiyo na kuwasaidia wagonjwa walemavu katika kufanya mazoezi pindi wanapohitaji huduma ya vifaa hivyo.
Alisema kushirikiana kujenga jamii ya Iringa ni jukumu la kila mwananchi hivyo vifaa vilivyoyolewa vitakuwa faida kwa kila mwanajamii na kuwataka kuendelea kutoa misaada katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...