KUNDI bingwa la miondoko ya mwambao, Jahazi
Modern Taarab litaanza kutambulisha nyimbo zake mpya mwishoni mwa mwezi huu
ambapo mji wa Morogoro utakuwa wa kwanza kupata uhondo huo.
Jahazi watafanya onyesho maalum mjini humo
Ijumaa ya Januari 31 ndani ya ukumbi wa Tanzanite Complex.
Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa Jahazi kupiga
ndani ya ukumbi huo uliofunguliwa kiasi cha mwaka mmoja uliopita.
Kwa mujibu wa mratibu wa onyesho hilo Warda Makongwa
wa Planet FM ya mjini humo, wameamua kuandaa onyesho hilo kufuatia maombi ya
mashabiki wengi waliotaka Jahazi nayo ibishe hodi ndani ya Tanzanite Complex.
Warda amesema Jahazi halitaenda hivi hivi bali
litaandamana na nyimbo mpya kabisa ambazo hazijawahi kusikika hapo kabla.
Amefafanua kuwa nyimbo hizo ni sehemu ya
maandalizi ya albam mpya ijayo ya Jahazi Modern Taarab inayoongozwa na Mfalme
Mzee Yussuf.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...