Ankal akiwa Trafalgar Square jijini London alikotembelea kwa vekesheni mwaka 1990... 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Looh, jamani vitambi hivi! Mungu wee! Hivi kwa nini ulituamuru kwamba tukishagonga miaka KADHAA basi lazima tupambane na hivi vitambi! Hebu muone hapo huyo Ankal enzi hizo alivyokuwa fit! Lakini ukimuona hivi sasa utadhani wametoka nyumba moja na mzee Mkapa! Mwee, jamani mwee! Life is so beautiful!

    ReplyDelete
  2. Aisee siamini anko umeanza kukwea pipa zamani hivyo. Aisee toka leo nakuheshimu. Tatizo anko uko simpo na huna majigambo kama watu fulani fulani ambao wangekuwa wewe saa hizi hatulali. Hongera sana sana anko, hii inadhihirisha juhudi binafsi na ubunifu unalipa. Sio mtu anategemea aidha jina la baba ama godfather ndio atanue mjini. Wewe ni mfano wa kuigwa katika ule usemi wa from rags to riches. Naunga mkono wadau waliotoa wazo la wewe kuandika kitabu cha maisha yako ili sisi na watoto wetu tuige. Dah mwana 90 mie nilikea nursery Aga Khan pale upanga, leo niko London miaka saba sasa lakini najiona bado kinda mbele yako...

    ReplyDelete
  3. Takriban miaka 24 si haba, kumbukumbu nzuri. Na mpaka leo hii, mtu aende LDN asipate ukodak Trafalgar Square, kwa nadra sana. Na hao njiwa wa wenzetu hawaogopi watu, tofauti na hawa wa kwetu, hawana kuingwa, washaruka zamani gani! Hawa 'Feral pigeons' wapo more friendly, nowadays wakuhesabu TS.

    ReplyDelete
  4. ANKAL halafu enzi hizo ulikuwa mrefu fulan hv , sasa urefu umeishia wapi?

    ReplyDelete
  5. wajameni, kweli tushazeeka, mwaka 90 wengine ndo kwanza mlikuwa vidudu, aka chekechea!, in the 90s Mi-stew alikuwa hana GARI, as a photojournalist he used to walk a lot from point A to B etc, doing his business of taking photos at the same time ( walking at 4mph burns 288 calories/hour), and mi-stew used to walk loads in the 80s and early 90s, moreover he is brown belt in Go jo-ryu, trained at Zanaki under sensei kamara bomani dojo(RIP).
    Tukicheza basketball Gymkhana michuzi na kamera yake akipita kupata taswira, na kwenye madisco yote ya dar Enzi zetu, space 1900, ymca, silver sands, jet club etc, remember shalamar, bob CHURA! those were the days.

    ReplyDelete
  6. mwee vitambi hivi ni janga la kitaifa..ankal ulikua bonge HB,figure mwake lakini sasa uko timu moja na akina mkapa,komba et al.mweee maisha haya.

    ReplyDelete
  7. Ankal you rock, simplicity, creativity, being humble and optimistic, respect for all irrespective of social status, race, creed etc have made you the media mogul in this country...This is similar to the "Down lane memory" creative work by TSN...Continue to teach people that human beings are trekking this world, it is only the legacy that matters, someday the future generations will cherish your great works to unite Tanzanians....

    ReplyDelete
  8. Hao njiwa wamependeza sana, bongo mikunguru tu haina hata adabu.

    ReplyDelete
  9. Mimi nauliza hivi hao kuku ni wa nani?

    ReplyDelete
  10. Mimi nimefurahishwa na hiyo mokasini uliyo vaa miguuni, ndio viatu vilisifika miaka hiyo, na mara zote inabidi uving'arishe.

    ReplyDelete
  11. Nadhani Ankali hii ndio ilukuwa mara yako ya kwanza kwenda Ulaya na kupanda ndege au siyo?

    Ni wazi ulipofika LONDRES yaani (London) kwa mara ya kwanza uliandaa na miche ya sabuni za Mbuni kwenye Begi lako ili uweze kufua nguo zikichafuka!!!

    ReplyDelete
  12. Mjomba inaelekea ulikesha na hukulala usiku wa kuamkia kupanda ndege kwa hii safari !

    ReplyDelete
  13. Ankali ktk begi lako la safari inaelekea ulifungasha vitu kibao kama ndio unahamia moja mkwa moja UK!

    Ulibeba taulo,(Koti la Khaki ni vile uliambiwa Ulaya kuna baridi), ndala, dawa ya mswaki na mswaki wa mti!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...