Mwenge wa Jumuiya ya Madola (Queens Baton Relay) utatembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili jumapili ya tarehe 19, Januari, 2014 kuanzia saa tatu kamili hadi saa nne asubuhi. 

Mwenge huo unatarajia kufika Hospitali ya Taifa Muhimbili ukiongozwa na Mheshimiwa Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Dianna Melrose.

Dhumuni la Mwenge huo kimataifa ni kutembelea nchi zote ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola katika kuhamasisha maandalizi ya Tamasha la Nne la Michezo na Utamaduni la Jumuiya ya Madola. 

Mwenge huu unakimbizwa kilomita 190,000 kupitia nchi 70 ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola. Safari ya mwisho ya Mwenge huu itakuwa Julai 23, 2014, Glasgow, Scotland kwa ajili ya ufunguzi wa sherehe za michezo ya 20 ya Jumuiya ya Madola.

Hii ni mara ya tano Mwenge huu kufika nchini Tanzania na utakuwa nchini kwa siku tatu ukisaidia kuhamasisha ushirikiano, kuimarisha umoja na, kuongeza ari ya wananchi hususani vijana waweze kuelewa nini maana ya michezo ya jumuiya ya madola.

Nia ya mwenge huu kuja Hospitali ya Taifa Muhimbili ni kutembelea watoto wanaougua saratani mbalimbali ili kuwapa matumaini ya kuishi na kwamba jamii inawanathamini. Watoto hawa watapata fursa ya kuushika mwenge huu na kupiga picha kama kumbukumbu muhimu katika maisha yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...