Mara baada ya kuundwa kwa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inayoongozwa na Katibu Mkuu Ndg. Abdulrahman Kinana mwanzoni mwaka mwaka jana, Sekretarieti hiyo imejiwekea utaratibu wa kufanya ziara mikoani kukutana na wananchi kusikiliza kero zao,kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuimarisha Chama mikoani. Utaratibu huu ni agizo la mkutano mkuu wa Taifa wa nane wa CCM uliofanyika Novemba 2012 mjini Dodoma. Nanukuu azimio hilo;
“ Chama Cha Mapinduzi lazima kiwe karibu na wananchi, kisikilize changamoto zao na kiwasemee wananchi na hasa wanyonge” Moja ya maazimio ya Mkutano Mkuu wa nane wa CCM 2012.
Kwa hiyo msingi wa kwanza wa ziara hizo ni maagizo ya Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambacho ndicho kikao cha juu kabisa cha Chama. Msingi wa pili ni ukweli kuwa CCM ndio iliyopewa dhamana na kuingia mkataba na wananchi kupitia ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015, hivyo inayowajibu wa kukagua utekelezaji wa ilani hiyo.
Na bila shaka wote tumeshuhudia jinsi ziara hizo zilivyoinua uhai wa Chama nchi nzima na kuongeza kasi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na kutatua kero mbalimbali za wananchi kwenye maeneo yao, kiasi cha kuongeza imani ya wananchi kwa CCM.
Unachokiongea kiko sahihi lakini mimi sikubaliani na njia uliyotumia.Kidogo haikuwa nzuri sana.Ilikuwa inawadhalilisha sana wale uliowataja pamoja na aliyewateua.Na mimi nawasifu viongozi wale na aliyewateua kwa kuwa watulivu na wakimya,walionyesha ukomavu wa hali ya juu..Siwatetei lakini kulikuwepo na njia nyingine za kutumia kupeleka ujumbe kwa aliyewateua badala ya kutumia majukwaa ya Siasa.Kwa UFUPI umepigwa goli la KISIGINO mkuu.
ReplyDeleteDavid V
The mdudu,anasema well said by Nape hiyo mizigo ilioachwa lazima itakua makini coz tunakokwenda ni sawa na vita ya NYOKA na KINYONGA ndugu zanguni kama kuna mdau yeyote ambae ashashuhudia ndondi za hao wadudu atakubaliana na mm,,maana kinyonga zile nguvu sijui huwa anazipata wapi? So kwa mtindo huu wa CCM kivumbi kipo,asanteni sn CCM mwendo Mchibuyu
ReplyDeleteThe mdudu,ww David V nilikua nakuheshimu sn lakini kwahizi pumba zako za leo nimekutoa kwenye kundi langu la watu wenye busara hao unaowatetea ndio wanaosababisha akina mama zetu na madada zetu kujifungua katika sakafu lo ushindwe ww na ulegee kama sufi
ReplyDelete