Leo asubuhi basi la abiria  la kampuni ya Mtei Express likitoka Sindida kwenda Arusha limechomwa moto na wananchi wenye hasira maeneo ya Njia panda Mnadani, mkoani Singida baada ya bus hilo kugonga pikipiki yaani bodaboda na kuua watu watatu hapo hapo. Zifuatazo ni taswira za basi hilo lililokuwa wakati na baada ya kuchomwa moto. 
Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Kaka Ankali nakuvulia kofia. Ndio maana kila mtu anaamini Blogu ya Jamii ni No. 1 blog Tanzania. Wengine ni photocopy tu. Habari hii nimeipata mchana wa leo, nikawa nasubiri ni chombo gani kitatuletea taswira. Nilipofungua Blogu ya Jamii I was not disappointed. Keep it up Bro!

    ReplyDelete
  2. Wanadhani wamemkomesha dereva/mmiliki. Hapo kampuni ya insurance inasikitika.

    ReplyDelete
  3. kwahio hao watu watatu waliopoteza maisha wamepona baada ya basi kuchomwa moto? Yaani watanzania tunasifika kwa upole na ukarimu ila ukiita mwizi papo hapo watu wanajeuka wauwaji, likipinduka gari la mafuta papo hapo watu wanageuka wezi na hapo kwenye ajali tayari wamehukumu na kuitekeleza hukumu yao.

    ReplyDelete
  4. Polisi,polisi,mko wapi mnalipwa mishahara ya walipa kodi lakini hamfanyi kazi yenu sawasawa.na dereva wa basi ugigonga mtu (binadamu) uliwapigia simu polisi au kama ulielewa kuwa utaharisha maisha yako pamoja na abiria kwa nini hukuendesha hadi kituo cha polisi kilicho kuwa karibu,lakini swaala la msingi ni kuwa raia wanachukua sheria mkononi kwa sababu hawana imani na polisi,

    ReplyDelete
  5. Poleni wafiwa.... "Basi likuwa na abiria 9 tuu" toka Singida kwenda Arusha.. Kasheshe mbona biashara kichaa au?

    ReplyDelete
  6. This is AFRICA, Karibu Tanzania nchi yenye Amani na Utulivu....hehehehee. kitu tit for tat, why mpka mahakamani watu wanamalizana hapo hapo, duh naona bado kitu stone age sijui?yani huwa nadata na hii nchi, ukienda kwa wataalamu utakuta wanaboronga mara ghorofa limeanguka, mara doctor kamkata mtu mguu instaead ya kumfanyia operation ya kichwa, wanasiasa naona ndio balaa kashfa kibao mara sijui kabaka katoto, but tupo karne hii hii ya 21. kweli hapa ni BONGO.

    ReplyDelete
  7. Lawlessness is a sign of failed systems and values.

    ReplyDelete
  8. Kutokuwanasheria ni ishara ya mporomoko wa nidhamu, dasturi na ustaarabu au stahamaki ya kuwepo nidhamu. Ni uhai wa kimsitu situ tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ombeni Mungu! Ktk kila jambo!

      Delete
    2. Ombeni Mungu. Kuepukana na kila jalibu

      Delete
    3. Si haki kuhua au kuchukua sheria mkononi

      Delete
  9. siasa hizi mbofu

    ReplyDelete
  10. tatizo wenye vyombo vikubwa kama mabasi ,malori na magari ya jeshi huwa wanamtindo wa kuwa na dharau kwa waenda miguu na wenye vyombo vidogo kama baiskeli pikipiki na magari madogo , kwa hio shingai kuona hatua hii waliochukua wananchi ni sawasawa itawatia akili wote wenye magari makubwa , pongezi kwa wale waliochoma , ikiwa tit fo tet sio nzuri mbona tukiangalia filamu mbalimbali stori zake mara nyingi huwa ni kulipiza kisasi kwa yule anayeonewa na sisi huwa tunashangilia na kufurahia wakati adui / dhalimu anapopewa kisago na yule aliyemuonea?

    ReplyDelete
  11. Jamani huu ni unyama gani! Bodabpda Ogopeni. Mwenyizi Mungu! Kwani ajali kama hii police ndio wahamuzi wetu na Mahakama kujua nani mwenye makosa ili awajibishwe hivyo Bodaboda kuchoma Gari ni kosa kubwa sana ktk jamii na mbele ya Mwenyezi MUNGU!

    ReplyDelete
  12. Mimi kila tukio siliangalii kijuu juu...swali ni why???????????

    Nadhani pamoja na kuwa huu ni uvunjifu mkubwa wa sheria; wananchi wamechoka na hawana imani na legal system; pqamoja na polisi...

    Kuna nchi kama Japan mimi nimesoma huko cha kwanza tulionywa tusiendeshe magari kwa kuwa tutajiweka kwenye hatari kwani ukigonga mtu mwanawani una miaka si chini ya 20 jela na kufidia familia yake....

    Hapa Tz as long as wewe ni dereva kugonga ni ajali kazini...utasikia 'hiyo ni traffic case'


    utadani ulikanyaga kuku...tujifunzee kwa hili...

    Sheria kali inaongeza umakini kwa madereva

    Matokeo ndio hayo watu wanaamua kuadhibu kivyao vyao maana hapo hakukuwa na case ya maana kwa dereva zaidi ya faini kama angekataa kutoa rushwa

    ReplyDelete
  13. Poleni. Sana! Si haki boda boda kujichukulia sheria mikononi wakati kuna vyombo vya dora Naomba serikari wote walio Usika na tukio hilo wawajibishe

    ReplyDelete
  14. Mdau Chife of manyemaJanuary 10, 2014

    Watu wote mnasema sheria za hao BODABODA mtu leo hii kaanunua pikipiki haendi kujifunza kwetaasisi za kuendesha chombo chochote hana license tayari yupo barabarani kwakweli wapewe elimu ya usalama barabarani kujua sio unaibuka hujui sheria wapi unahitajika kupiga overtake pia unapopiga overtake unahakikisha umbali gani umemeishana na bus au gali kubwa usipunguze speed keep going sheria za usalama wa abiria ziludiwe hususani bodaboda
    Mdau UK chef wa kimayema

    ReplyDelete
  15. Nje kidogo ya Mada.Ankal kuna mdau(na wadau wengine) juzi humu alikuwa analalamika kwa alipaki gari kidogo kwenda kununua dawa Famasia,akakuta gari lake limefungwa chuma na kudaiwa Faini laki 1.Sasa mwambie serikali ya CCM ina masikio bwana,imesikia sauti zetu.Mkuu wa mkoa wa Daresalaam amepiga marufuku yale makampuni yote yaliyokuwa yananyanyasa wananchi na hizo wrong parking sizizo na mashiko(Mikataba yao imevunjwa!!).Comment zetu huwa zinasomwa na wahusika,Blog ya Jamii OYEEEEEEE

    David V

    ReplyDelete
  16. Street justice

    ReplyDelete
  17. hii ndio tanzania na hii ndio singida daily inasifika kwa kuchoma mabasi tunakwenda wap jamani??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...