Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, Dkt. Adelhelm Meru (kulia) akielezea jambo kwa Naibu Waziri wa
Biashara na Viwanda wa Afrika ya Kusini, Bi. Elizabeth Thabethe (katikati) na Balozi wa Afrika
ya Kusini nchini Tanzania, Bw. Thanduyise Chiliza (kushoto). Ujumbe wa maafisa mbalimbali
uliitembelea EPZA jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, Dkt. Adelhelm Meru (kulia) na Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa
Kiwanda cha nguo cha Tanzania Tooku Garments Ltd, Bw. Rigobert Massawe (wa pili kulia)
wakitoa zawadi kwa Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda wa Afrika ya Kusini, Bi. Elizabeth
Thabethe (kushoto) wakati ujumbe huo ulipotembelea kiwanda hicho kilicho ndani ya eneo la
EPZA jana. Wa pili kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Bi. Radhia Msuya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...