Viongozi wa dini wametembelea Bomba Jipya la Gesi asilia la Mtwara- Dar
es Salaam, mtambo wa kusafisha umeme wa Mnazi Bay na maeneo mengine
mbalimbali ya uendelezaji wa gesi asilia katika Mkoa wa Lindi na Mtwara.
Viongozi hao wamefanya ziara hiyo ikiwa ni maandalizi kabla ya kufanyika
Kongamano la Viongozi wa dini linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam
tarehe 21 na 22 mwezi Januari, 2014.
Ujumbe wa Viongozi wa dini wakiangalia mojawapo ya visima vya nchi kavu vya
kusafisha gesi katika eneo la Mnazi Bay, Mtwara.
Viongozi wa dini wakipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Masuala ya gesi na
Msimamizi Mkuu wa Mitambo ya kusafisha gesi Mhandisi Sultan Pwaga katika
eneo la Madimba kinapojengwa Kiwanda cha kutakasa Gesi.
Mafundi wa Kampuni ya China Petroleum Pipline (CPP) wakiendelea na kazi ya
kuunganisha mambomba ya gesi katika kambi ya Madangwa.
Meneja Mradi wa Bomba la gesi kutoka Da r es Salaam hadi Mtwara Mhandisi
Kapuulya Musomba akiwaeleza viongozi wa hatua mbalimbali zilizofikiwa katika
utekelezaji wa Mradi huo. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na
Madini Mhandisi Ngosi Mwihava.
Usalama wa Bomba la Gesi dhidi ya hujuma:
ReplyDeleteMambo mawili hapa chini ni muhimu sana,
1.Njia nzima linamopita Bomba la Gesi yawekwe makubaliano na google Satelite map, ili waiingize ktk Ramani na camera kwa kila dakika inayokwenda.
2.Iwekwe ktk Makubaliano na FLUID LEAKING TECHNOLOGY yaani Taasisi inayotoa Tekinolojia ya uvujai wa vitu vya gesi/ hewa na maji Mamlaka inaweka software zao ku detect tukio lilipotokea na kutuma mawimbi ya taarifa kwenye Kituo.
Bila ya hatua hizi mbili hata kwa gharama kidogo nina wasiwasi na usalama wa bomba la gesi dhidi ya hujuma kwa kuwa maeneo mengine linapita misituni kabisa!!!
Mdau wa kwanza:
ReplyDeleteHilo ni muhimu kulingana na uzito wa suala lenyewe na jinsi changamoto zilivyo jitokeza hasa kwa wakazi wa eneo hilo la mikoa linakopita Bomba la Gesi kuhusiana na mpango huu.
Mdau wa kwanza,
ReplyDeleteNi kweli kabisa kwa kuwa hata ktk familia mtazaliwa wengi lakini hapawezekani kila mmoja akawa na akili timamu lazima moja wapo litakuwa NDONDO tu!
Ndio hivyo hivyo hata kwenye nchi, hamuwezi wote kuwa na akili nzuri lazima utakuta panajitokeza Miteja na Mivibaka ya kuiba hadi mifuniko ya mitaro ya majitaka barabarani, kung'oa mataruma ya Reli na mawaya ya transfoma kuwenda kuuza Skrepa!