Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi ya Isilowaya iliyoko kata ya Ilula wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wakiwa wamekaa katika baadhi ya madawati 30 yaliyotolewa na Faidika. (Picha na Denis Mlowe)
======= ====== ========
WAASWA KUACHA KUSUBIRI WAHISANI KUTOA MISAADA
Na Denis Mlowe,Iringa.
WATANZANIA wametakiwa kujenga utamaduni wa kumaliza matatizo yao ya ndani badala ya kusubiri wahisani kufanya hivyo kama sehemu ya kushiriki moja kwa moja katika juhudi za ujenzi wa Taifa .
Changamoto hiyo imetolewa Meneja wa mikoa ya Iringa na Njombe wa Taasisi mikopo Faidika, Elisha Mboka wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa madawati 30 yenye thamani ya shilingi milioni 3 kwa shule ya msingi ya Isoliwaya iliyopo kata ya Ilula mkoani Iringa.
Mboka alisema wakati umefika sasa kwa watanzania kuona umuhimu kusaidia juhudi za kumaliza changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii badala ya kuendelea kuwa tegemezi kwa misaada ya wahisani ambayo siku zote inakuwa na masharti ndani yake.
"Ndugu zangu sisi kama watanzania na kama sehemu ya jamii hii hatuna budi kutoa mchango wa dhati kwa taifa letu na jamii yetu. hakuna siku mtu kutoka nje ya jamii yetu na taifa letu atawajibika moja kwa moja na matatizo yetu. ni lazima tuwe wazalendo na kuepuka kuwa wanafiki kwa maendeleo yetu wenyewe"
Aidha aliitaka Serikali na jamii kwa ujumla kuelekeza juhudi zake katika maboresho ya mfumo wa elimu nchini kwani kwa kufanya kutasaidia tanzania kupiga hatua za kimaendeleo kwa haraka zaidi kuliko ilivyo sasa.
kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya Isoliwaya Asifiwe Mwagike alisema kwa muda mrefu shule yake imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya upungufu wa madawati, matundu ya vyoo na nyumba za walimu na kuwashukuru shirika la Faidika kwa msaada huo wa madawati.
Sikuhizi kila dawati la shule ya msingi mbele utaona chata la mhisani.....ngoja na mie nije nitoe .....sideboy wa kitaa.
ReplyDelete